BATULI AMPINGA WEMA, ‘WASANII TULIOSHIRIKI KAMPENI ZA CCM TULILIPWA NA MIKATABA IPO’

Msanii wa Filamu nchini, Batuli aliyeshiriki kampeni ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya ‘Mama ongea na Mwanao’ amekanusha taarifa zinazoeleza kuwa wasanii walioshiriki kampeni hiyo hawakulipwa.
Batuli amesema taarifa hizo siyo za kweli na kueleza kuwa CCM iliwalipa wasanii wote walioshiriki katika kampeni ya ‘Mama Ongea na Mwanao’ na mikataba ya malipo hayo ipo.
“Nakanusha taarifa za kwamba wasanii tulioshiriki kampeni za CCM ‘Mama ongea na mwanao’ hatukulipwa, tulilipwa na mikataba ipo” amesema Batuli
Batuli amesema hayo leo Februari 28, 2017 wakati akizungumza na waandishi wa habari, kufuatia taarifa ya msanii wa filamu, Wema Sepetu kuwa wanaidai CCM fedha za kampeni. Wema alinukuliwa akiongea hayo wakati akitangaza kujiengua katika chama hicho na kuhamia Chadema.
Batuli amesema kuwa haiwezekani msanii mkubwa hivyo asema hakulipwa wakati yeye ndio alikuwa anawalipa wasanii wengine.
“Haiwezekani wewe staa mkubwa unasema haujalipwa, wakati wewe ndio ulikuwa unalipa watu” amesema Batuli
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post