DOGO JANJA AMTUMIA UJUMBE MZITO MAKONDA

Msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende maarufu kama Dogo Janja, amefanyiwa tukio la wizi usiku wa kuamkia leo, kutokana na kukerwa kwa tukio hilo ametumia  ukarasa wake wa instagram kuandika waraka kwa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda kuliangazia swala la wezi jijini Dar es salaam.
Hitmaker huyo wa ‘Kidebe’ katika ujumbe wake alianza kwa kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kazi kubwa alinoifanya kuhusiana na madawa ya kulevya na amekiri matunda ya vita hiyo yanaonekana wazi.
Pia Dogo Janja amemuomba Mkuu wa Mkoa kuangalia swala zima la wezi kwani limeonekana kukithiri katika baadhi ya maeneo, usiku wa kuamkia leo Dogo Janja ameibiwa baadhi ya vitu kwenye gari lake aina ya Porte ikiwemo taa, radio na power window.
Kupitia kurasa wake wa istagram Dogo Janja ameandika haya, mlengwa mku akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.
”Muheshimiwa makonda tunashkuru umelisimamia vizur swala la madawa ya kulevya na tumeona matunda yake..lakin bado kuna hili la hawa wezi wa vipuli vya magari km taa radio powerwindow naona km alijaongelewa ivi..awa jamaa wapo wengi sana mjini na wanajulikana..wanakuibia alafu wanakupigia cm wapi pakuvipata vitu vyako..mueshimiwa tuanzishe na kampeni hii tupunguze kutiana hasara..kigali changu chenyewe ndio hiki nataftia riziki jana ucku wamekuja wameiba kila kitu radio taa za mbele na nyuma..ntatokaje kujitaftia rizik? Cc: @paulmakonda.”

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post