RIDHIWANI AANIKA UHUSIANO WA JK NA LOWASSA, JK ALICHOMWAMBIA ALIPOIONA PICHA YAO

SHARE:

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni mtoto wa rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete ameeleza uhusiano uliopo kati ya baba yake...

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni mtoto wa rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete ameeleza uhusiano uliopo kati ya baba yake na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa bado ni maswahiba.
Ridhiwani ametoa ufafanuzi huo kutokana na imani iliyojengeka kuwa kuna uhasama kati ya Dkt. Kikwete na Lowassa ambao awali walikuwa maswahiba wakubwa kabla ya siasa kuingiza doa kwenye uhusiano huo. Uhasama huo uliaminika kuwepo na kuongezeka hasa baada ya Dkt. Kikwete kuongoza kamati ya maadili ya CCM iliyoliondoa jina la Lowassa katika orodha ya waliokuwa wakiwania nafasi ya kugombea urais, hali iliyopelekea mwanasiasa huyo kuhamia Chadema na kugombea nafasi hiyo.
Akizungumza wikendi hii na mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo baada ya kuenea mitandaoni picha inayomuonesha akisalimiana na kuteta na Lowassa, Ridhiwani alieleza kuwa hakuna uhasama kati ya baba yake na mwanasiasa huyo mkongwe kama wengi wanavyoamini.
Aliongeza kuwa amewahi kuwashuhudia wakizungumza na kuwasiliana kama kawaida kwa njia ya simu mara kadhaa.
“Kwanza hakuna ugomvi kati ya watu hawa wawili. Unajua watu wanashindwa kuelewa kwamba hakuna urafiki katika masuala ya kazi. Kwa mfano suala lile la kumtafuta rais, jambo la kutafuta rais sio jambo la Jakaya peke yake,” alisema Ridhiwani.
“Ukweli wa mambo ni kwamba Bwana Lowassa na bwana Kikwete ni watu wanaosaidiana katika mambo mengi sana,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, Ridhiwani alieleza kuwa baba yake alipoona picha yake na Lowassa wakisalimiana baada ya kukutana Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa kwenye mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga alimpigia simu kutoka Ethiopia na kumtaka kuendelea na hali hiyo kwani siasa sio vita.
“Kwa mfano hata jana jioni alinipigia simu, of course alikuwa yuko Ethiopia, akaniambia ‘bwana nimeona kwenye picha uko na bwana Edward [Lowassa] ilikuwa wapi hapo?’, nikamwambia nimekutana nae uwanja wa Taifa tulikuwa tunaangalia mpira,” “[Akasema] ‘aah naye alikuja kuangalia mpira’ nikasema ndio. Akasema ‘okay hayo ndio mambo mnayotakiwa kufanya, msifike sehemu mkaona kama siasa ni vita’.
“Kwahiyo ndio maana mimi baada ya kuongea naye akaniambia siasa sio vita, na mimi niliposhika simu yangu Instagram yangu nikaandika kwamba ‘tunaendelea kujifunza…. Lakini basically najifunza kutoka kwa maneno ya mzee wangu ambaye ameniambia kwamba ‘siasa sio vita na kwamba na ninyi katika umri wenu inabidi muendelee kujifunza’ kwahiyo hata mimi comment yangu kwenye Instagram, actually sababu yake kubwa ni hiyo,” alifafanua.
Ridhiwani alieleza kuwa alimuona Lowassa baada ya kipindi kirefu kupita hivyo aliamua kumfuata na kumsalimia ambapo pamoja na mambo mengine, Lowassa alimuuliza alipo Dkt. Kikwete na akampa salamu zake amfikishie na familia kwa ujumla.
Lowassa alilazimika kujiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu mwaka 2008 katika Serikali ya Awamu ya Nne iliyokuwa inaongozwa na Dkt. Kikwete kutokana na sakata la Richmond.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: RIDHIWANI AANIKA UHUSIANO WA JK NA LOWASSA, JK ALICHOMWAMBIA ALIPOIONA PICHA YAO
RIDHIWANI AANIKA UHUSIANO WA JK NA LOWASSA, JK ALICHOMWAMBIA ALIPOIONA PICHA YAO
https://4.bp.blogspot.com/-WmK1rRedzyg/WLUegqweJ2I/AAAAAAAAW6k/nYmIIB7pGwQUkqKoffHEFCz1TAJfuMgoQCLcB/s1600/JK-na-Lowassa.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-WmK1rRedzyg/WLUegqweJ2I/AAAAAAAAW6k/nYmIIB7pGwQUkqKoffHEFCz1TAJfuMgoQCLcB/s72-c/JK-na-Lowassa.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/02/ridhiwani-aanika-uhusiano-wa-jk-na.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/02/ridhiwani-aanika-uhusiano-wa-jk-na.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy