RIDHIWANI AELEZA ALICHOTETA NA LOWASSA ,JK AMPIGIA SIMU

SHARE:

Dar es Salaam. Picha inayomuonyesha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiteta jambo na Ridhiwani, mtoto wa Rais wa Serikali ya Awamu...

Dar es Salaam. Picha inayomuonyesha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiteta jambo na Ridhiwani, mtoto wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete imemfanya mbunge huyo wa Chalinze kujitokeza na kuizungumzia.
Lakini yapo matukio mengi yanayoonyesha “siasa si uhasama” kama alivyosema Ridhiwani, Mwananchi imezungumza na Ridhiwani kuhusu walichoteta na Lowassa na pia inakurejeshea kumbukumbu za wanasiasa walionekana kuwa na uadui, lakini nje ya jukwaa wanaelewana.
Picha ya Ridhiwani na Lowassa ilipigwa wakati wa mechi ya watani wa jadi katika soka nchini, Simba na Yanga iliyofanyika Uwanja wa Taifa Jumamosi iliyopita na kuhudhuriwa na maelfu ya watu, wakiwamo wanasiasa ambao walikaa jukwaa kuu na kubadilishana mawazo bila kujali tofauti zao.
Katika picha hiyo, Ridhiwani, akiwa amevalia fulana ya njano anaonekana akiwa amemuinamia Lowassa ambaye amekaa, wakionekana kuteta jambo huku wameshikana mkono. Wote wawili wanaonekana kutabasamu.
Wawili hao walionekana kuwa na uadui mkubwa kabla ya kuanza kwa mchakato wa kutafuta mgombea urais wa CCM, huku Ridhiwani akionekana kutomkubali mbunge huyo wa zamani wa Monduli, ingawa hakuwahi kusema hadharani.
Wakati fulani mitandao ilidai kuwa Ridhiwani amesema nchi haiwezi kuongozwa na mtu kutoka Kaskazini, tuhuma alizozikanusha. Katika mahojiano na Mwananchi yaliyofanyika kipindi hicho, Ridhiwani alitaja makada watano waliofungiwa kwa miezi 12 na CCM kujishughulisha na kampeni, kuwa walikuwa na sifa ya kugombea urais.
Lowassa alikuwa mmoja wa makada hao. Lowassa hakujitokeza kupambana na Ridhiwani, ingawa ilikuwa inasemekana kuwa wana uadui mkubwa.
Lakini hali hiyo haikuonekana wakati wanasiasa hao walipokutana Uwanja wa Taifa Jumamosi.
Faragha ya Lowassa na Ridhiwani
“Unajua ni siku nyingi (sikuwa nimekutana na Lowassa) na nilikuwa nimemkumbuka sana. Mkutano wa Dodoma (wa mwaka 2015), alikuwa amekaa na (aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Hamis) Mgeja. Kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi nikamsalimia ‘mzee shikamoo’. Akanijibu ‘marahaba mwanangu, hujambo?’ Nikamwambia ‘sijambo’,” alisema Ridhiwani akirejea mazungumzo yake na Lowassa katika Uwanja wa Taifa.
Ridhiwani alisema baada ya salamu ile, alihitaji kufahamu zaidi kuhusu Kikwete.
“Akaniuliza pale kwamba ‘baba yako yuko wapi?’ Nikamwambia ‘yupo anaendelea vizuri, lakini kwa sasa amesafiri kikazi yuko Ethiopia’. Basi akaniambia akirudi nimsalimie sana, na mie nikamjibu nitamfikishia salamu huku tunafurahi pale.”
Katika kumalizia maongezi hayo, Ridhiwani alisema alimkaribisha Lowassa mpirani.
“Akasema ‘unajua sisi watu wa mpira ila shughuli tu ndiyo zinatubana’. Tukafurahi pale, akasema asante sana basi nikarudi kukaa kwenye nafasi yangu,” alisema Ridhiwani.
Katika ujumbe wake aliouandika katika akaunti yake ya instagram, Ridhiwani anaonekana kujifunza jambo baada ya kumalizika kwa siasa za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
“Siasa ni shule ambayo haina mwisho. Nahisi bado niko shule ya msingi na ninaendelea kujifunza.” ameandika Ridhiwani katika akaunti hiyo.
Akiongea na Ayo Tv baadaye juzi, Ridhiwani alisema baada ya picha ile kusambaa, baba yake alimpigia simu na kumuuliza kuhusu tukio la kukutana na Lowassa.
“Jana (juzi) jioni (Kikwete) alinipigia simu akiwa Ethiopia, akaniuliza ‘bwana nimeona kwenye picha uko na Bwana Edward’. Nikamwambia ‘eh (ndiyo), nilikutana naye Uwanja wa Taifa tulikuwa tunaangalia mpira’. Akaniuliza ‘naye alikuja kuangalia mpira? nikasema, eeh,” alisimulia Ridhiwani katika mahojiano hayo.
“Akasema ‘ok sawa bwana. Hayo ndiyo mambo mnatakiwa mfanye. Msifike sehemu mkaona siasa ni vita’. Ndiyo maana baada ya miye kuongea naye na kuniambia siasa siyo vita, nikatuma ujumbe ule.
“Nikaingia kwenye ukurasa wangu pale nikasema tutaendelea kujifunza, lakini basically ninajifunza kupitia maneno ya mzee wangu (Jakaya Kikwete), aliniambia kwamba na ‘nyinyi katika umri wenu muwe peace kuendelea kujifunza, ndiyo maana nikaeleza comment yake.”
Lowassa, ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Kikwete tangu walipogombea urais kwa mara ya kwanza mwaka 1995 na baadaye kwa mafanikio mwaka 2005, alitofautiana na rafiki huyo baada ya kuenguliwa jina lake mwaka juzi na kuhamia Chadema, ambako alipewa fursa ya kugombea urais na kushika nafasi ya pili.
Tangu kumalizika kwa uchaguzi huo, uhusiano baina ya wanasiasa wa vyama vya upinzani na CCM umekuwa mbaya na wakati fulani walianza kutosalimiana wakati wakiwa bungeni.
Masuala hayo ya kisiasa pia yaliwafanya hata wanasiasa wa upinzani kutoelewana.
Wakati huo wa kuelekea Uchaguzi Mkuu uliopita, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM wakati huo, Nape Nnauye alikuwa akimrushia vijembe kadhaa Lowassa. Lowassa hakuwa akimjibu na wakati fulani akiwa Dodoma alisema kuna mtu ambaye amekuwa akimtuhumu mambo mengi, lakini hangeweza “kumjibu kwa kuwa atampa umaarufu”.
Lakini wawili hao wamekuwa wakionekana wakizungumza pamoja katika hafla tofauti tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.
Wengine walioingia kwenye mzozo wa kurushiana maneno makali ni Nape na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe. Tofauti zao zilikuwa bayana wakati wa kupitisha Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari, ambao Zitto aliupinga kwa kutojali maoni ya wadau.
Akitumia maneno makali, Nape alieleza kumshangaa Zitto akisema hajui alikuwa akizungumzia muswada gani, lakini mbunge huyo wa Kigoma alieleza kuwa anachotaka ni hoja kujibiwa na si kuzungumzia watu.
Upinzani kama huo ulionekana bayana kwa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Zitto wakati chama hicho kikijiandaa kwa uchaguzi wa viongozi wake.
Zitto alieleza matamanio yake ya kugombea uenyekiti wa Chadema, lakini baadaye akaingia kwenye tuhuma za kutaka kufanya mapinduzi kabla ya kusimamishwa.
Akiwa amesimamishwa, Zitto na viongozi wa Chadema walirushiana maneno mabaya, kiasi cha kufikia kupachikana majina yanahusishwa na kashfa zilizokuwa zimelikumba taifa wakati huo pamoja na ubadhirifu ndani ya chama hicho.
Hata hivyo, Zitto alijitokeza baadaye na kusema kuwa hana matatizo na Mbowe na hivi karibuni wamekuwa wakionekana katika matukio tofauti, hasa kutokana na hisia kuwa kuna njama za kuua upinzani.
Wakati mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alipomtaka Mbowe na watu wengine 64 waripoti kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya, Zitto aliambatana na kiongozi huyo wa kambi ya upinzani katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo.
“Naamini shambulio dhidi ya Mbowe, si shambulio kwa Chadema pekee, bali kwa upinzani wote,” alisema Zitto katika mkutano huo akitumia lugha ya Kiingereza.
“Mimi nimefanya kazi na Mbowe. Ameniibua nikiwa mdogo kabisa chuo kikuu. Kama angekuwa akifanya biashara ya dawa za kulevya, mimi ndiye ningekuwa punda wake.
“Kwa hiyo mtu anapoibuka na kutoa tuhuma kubwa kama hizo, ni kitu ambacho kinapaswa kulaaniwa si tu na sisi wanasiasa wenzake, bali hata nyinyi wenye kalamu waandishi. Kwasababu nani anayejua Makonda ataishia wapi.”
Zitto alimhakikishia Mbowe kuwa atamuunga mkono na kwamba alienda kwenye mkutano huo kuonyesha mshikamano.
Katika ukurasa wake wa facebook wakati wa sakata hilo, Zitto alizungumzia kitendo chake akisema itakuwa ni ujinga kwa mtu kuendelea kushikilia msimamo wake hata katika mambo ya msingi. Alisema msimamo unaendana na hali ilivyo, akimaanisha hali ya kisiasa ya sasa inayolazimisha wapinani kuondoa tofauti zao.
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alikuwa akipishana kwa kauli na Spika wa Bunge la Kumi, Anna Makinda na wakati fulani ilionekana kama watu ambao wasingeweza kukutana na kufurahi pamoja.
Wakati wa vikao vya Bunge, Lissu alikuwa akihoji utendaji wa Makinda, ambaye hata hivyo alikuwa akitumia uzoefu wake kumdhibiti. Mara kadhaa Lissu alibishia amri za Makinda za kutaka akae na wakati mwingine kumtaka afute maneno yake.
“Najua Tundu Lissu anazifahamu kanuni na taratibu, lakini akiamua kuzikunja, anazikunja,” alisema Makinda wakati mwanasheria huyo mkuu wa Chadema akitoa maoni ya upinzani kuhusu muswada wa sheria wa marekebisho ya sheria.
Lakini katika burudani, Lissu na Makinda walikuwa pamoja wakicheza muziki huku wakiwa wameshikana, mithili ya marafiki wawili walioelewana kwa muda mrefu.
Wapinzani pia walitofautiana wakati mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alipofungua kesi Mahakama Kuu kupinga ushindi wa Halima Mdee katika uchaguzi wa ubunge wa Kawe mwaka 2010.
Mbatia alifungua kesi hiyo dhidi ya Mdee, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi, akilalamika kuwa katika mikutano ya kampeni Mdee alimuita kuwa ni “fataki” anayefanya mapenzi na watoto wa shule, kibaraka wa CCM na kwamba alikuwa akilipwa Sh80 milioni kila wiki na CCM
Hali haikuwa nzuri kwa Mdee na Mbatia hadi vyama vyao vilipokutana kujadili suala hilo na baadaye kukubaliana kufuta kesi hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari alisema ni kweli siasa si vita, lakini kwa hapa nchini siasa imegeuka kuwa vita. Alisema Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi za kiafrika zinazoendesha siasa kama vita.
Alisema tangu uongozi wa awamu ya tano ulipoingia madarakani, kuna zaidi ya wanachama 250 waliofunguliwa mashtaka na kuwekwa rumande kwa madai ya kesi za uchochezi.
“He was right, watu wanahoji eti inakuwaje anapiga picha na Lowassa ambaye hakuwa na mahusiano mazuri na baba yake. Hapana wanakosea, siasa si vita kwa watu waungwana, lakini ni si kwa watwana,” alisema Profesa.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: RIDHIWANI AELEZA ALICHOTETA NA LOWASSA ,JK AMPIGIA SIMU
RIDHIWANI AELEZA ALICHOTETA NA LOWASSA ,JK AMPIGIA SIMU
https://4.bp.blogspot.com/-a_K3SVeXdKM/WLUaEtf6xtI/AAAAAAAAAw4/xkg76KYhjhcA-NpirQxxPjwfxN4OOuFKwCLcB/s640/pic%252Bridhiwani%252Bateta.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-a_K3SVeXdKM/WLUaEtf6xtI/AAAAAAAAAw4/xkg76KYhjhcA-NpirQxxPjwfxN4OOuFKwCLcB/s72-c/pic%252Bridhiwani%252Bateta.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/02/ridhiwani-aeleza-alichoteta-na-lowassa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/02/ridhiwani-aeleza-alichoteta-na-lowassa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy