ALICHOANDIKA IRENE UWOYA KUHUSU WADADA WA BONGO MOVIE WANAOJIINGIZA KWENYE SIASA KIMASLAHI

Movie ilianza baada tu ya mwanadada Wema Sepetu kutangaza kuwa amehamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akitokea CCM ndipo drama za baadhi ya wadada hao wa Bongo Movie waliohusika katika kampeni za Mama Ongea na Mwanao kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka 2015 zilipoanza.
Ambapo ilisikika kuwa Wema Sepetu alidai kwamba CCM haikumlipa hatashilingi wakati yeye anafanya kampeni hizo na baadae Batuli ambaye ndiye makamu mwenyekiti wa kikundi hicho kufunguka na kukanusha vikali madai hayo ya Wema Sepetu kwamba hajalipwa pesa.


Baada ya mapicha picha yote hayo, muigizaji Irene Uwoya aliona sio kesi na kuingia katika page yake ya Instagram na kuandika kile ambacho anakiona kuwa ni sahihi kwa drama zinazoendelea mitandaoni.
Ndipo alipoamua kuporomosha ujumbe mrefu ulioambatana na picha yake katika page yake hiyo ya Instagram.
Ujumbe ambao ulisomeka kama ifuatavyo.
“Katika maisha siku zote ushauri unaruhusiwa kutolewa au kupokelewa… Lakin sio lazima mtu kupokea ushauri unaotolewa… Kila mtu anauhuru wakuamua kitu ambacho anahisi kinamfaa kwenye maisha sababu… Sazingine kwenye maisha Kuna sehemu inafika unacho jiskia kwenye moyo wako sio rahisi mtu mwingine kujiskia … Sasa ni mbaya sana kuishi kwa hisia… Ifikie Wakati tujitaidi kuheshimu hisia Za mtu… Lakin pia kunavitu vingine nazani Nivyema vkabaki kwa wausika wavinaowahusu…yani sio lazima kuongea kila kitu kwenye jamiii… Watu wanatamani sazingine kuskia vtu ambavyo wanahisi vinafaida kwa Jamaniii… Kunavitu vingine ukiongea havina maana… Mfano mim ni CCM damu… Lakin kunavitu vinaboa sanaaa Kweli kada mzima wa CCM unasimama hazarani unasema tulilipwa kufanya campaign? hatakama lakini unafundisha Nin Jamiii? Unafundisha jamiii kwamba yote tuliyoongea kuhusu CCM hatukuyaamanisha nikwasababu tulilipwa? Unaiambia jamiii ulikuwa tayari kuwadanganya na mliwadanganya sababu mlilipwa? Hivi Kweli? Kwahiyo jamiii ione Chochote Tutachoonge wasikiamini maana yake tutakuwa tumelipwa? Kwahiyo ata mnayoyaongea mnataka kusema mmelipwa? Minazani tujifunze kunyamaza sazingine kama hamna ulazima wakuongea mnaweza kuhisi mmnajenga kumbe mnaharibu kabisaaa… Embu Tufanye Kazi zinazo tuhusu Jamaniii… Nigeria wenzetu sasa wako Hollywood wanaigiza huko… Sisi ata nigeria kwenyewe bado hatuja pasua… Lakin hapa Tupo busy kushabikia ujinga na vitu vya kipumbafu na visivyo na Msaada kwajamiii… Kwastaili hiii… Hollywood tutaiskia na kuiona kwenye TV.no”
Wapo ambao wameyachukulia maneno ya Irene kama maneno ya hekima na kuhisi kwamba ameona mbali zaidi, na pia wapo ambao wameichukulia kama kutafuta kiki. Vipi kuhusu wewe? Una mawazo gani juu ya alichokiandika Irene Uwoya? Niandikie hapa kwenye comments.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post