ALICHOANDIKA SHYROSE BHANJI BAADA YA CCM KUKATA JINA LAKE UBUNGE AFRIKA MASHARIKI

Aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shy-Rose Bhanji amelalamika jina lake kukatwa katika kinyang’anyiro cha kutetea nafasi hiyo katika muhula ujao bila kuhojiwa juu ya tuhuma zilizopeleka jina lake kukatwa.
Licha ya malalamiko hayo, pia Shy-Rose Bhanji ametumia fursa hiyo kuwapongeza watu waliochaguliwa kuwa wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi na kuwashukuru wabunge kwa kumpigia kura zilizomuwezesha kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa mwanzo waliopata kura nyingi zaidi.
Shy-Rose ametoa malalamiko hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika;
“Ingawa jina langu limekatwa na Kamati Kuu ya Chama bila ya mimi nwenyewe kuitwa na kuhojiwa ili nipewe haki ya kujibu hoja zozote dhidi yangu, nawapongeza wote waliochaguliwa kuwa wagombea wa EALA kupitia CCM. Ninawashukuru sana Wabunge kwa kunipigia kura nyingi zilizoniwezesha kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa mwanzo walioongoza kwa kura.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post