ARNOLD SCHWARZENEGGER AJITOA KUONGOZA KIPINDI CHA CELEBRITY APPRENTICE

Aliyekuwa Gavana wa California Arnold Schwarzenegger ameiambia CNN kuwa hatorejea kuongoza kipindi cha The Celebrity Apprentice kilichokuwa kikiendeshwa na rais Donald Trump.

Schwarzenegger amesema anaachana na kipindi hicho kinachoangalia uwezo wa kusimamia fedha wa washiriki, kwa kile alichodai kuwa ni kuchafuliwa na uhusika wa Trump.

Amesema kuwa kipindi hicho kinachorushwa na kituo na NBC kimekuwa kikishuka idadi ya watu wanaokiangalia kutokana na Trump kutokubalika sera zake urais.

Trump ambaye aliachana na kipindi hicho ili kugombea urais, amekuwa akiwakosoa watu aliowaachia kukiendesha kipindi hicho.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post