ASKARI WA JWTZ AHUKUMIWA KIFUNGO KWA KUMUUA MWENZAKE

MAHAKAMA kuu kanda ya Tabora, imemhukumu askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) private Yusuph Haji, kifungo cha miaka mitano jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua askari mwenzake Hildefonce Masanja kwa kumpiga risasi pasipo kukusudia.
Hukumu hiyo illitolewa na Jaji wa mahakama hiyo, Sam Rumanyika baada ya ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo. Jaji Rumanyika alisema adhabu hiyo imetolewa ili iwe fundisho  kwa mshtakiwa pamoja na wengine wenye tabia kama hiyo.
Aliongeza kuwa upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi sita waliothibitisha kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo. Akisoma hukumu hiyo, Jaji Rumanyika alisema kuwa Mshtakiwa akiwa amelewa aliingia chumba cha kuhifadhia silaha na kuchukua bunduki kisha kumpiga nayo mwenzake Masanja na kufariki dunia.
Wakili wa kujitegemea wa upande wa mshtakiwa aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu mteja wake kwa madai kuwa amekaa mahabusu kwa muda mrefu tokea mwaka 2009 na pia anayo familia inayomtegemea.
Mahakama ilitupilia mbali uamuzi huo na kutoa adhabu hiyo ya miaka mitano jela.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post