ASKOFU GWAJIMA AFANYIWA UPEKUZI NYUMBANI KWAKE

Wakili  wa Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na uzima, Askofu Josephati Gwajima,  Peter Kibatala amesema kuwa polisi wamefanya upekuzi kwa mara nyingine nyumbani kwa Askofu huyo.
Kibatala ambaye ni wakili wa Askofu Gwajima amesema kuwa mbali na kupekuwa nakupiga picha kila kona ya nyumba pia walikwenda katika kanisa lake lililopo Ubungo kwa ajili ya upekuzi.
“Waache wafanye yao na sisi tutafanya yetu kisheria, Kwani hatuwezi kuwazuia Polisi kufanya shughuli yao na baada ya kumaliza na sisi tutajua nini cha kufanya,” amesema Kibatala.
Msemaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, David Mngongolwa amesema Gwajima alikwenda polisi kuripoti kama alivyoamriwa kufanya hivyo.
Aidha, Mngongolwa ameongeza kuwa baada ya kuripoti askari walimchukua na kwenda naye nyumbani kwake kwa ajili ya upekuzi na baada ya hapo waliondoka naye.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda amesema hana taarifa za kukamatwa kwa Gwajima kwa maelezo kuwa alikuwa katika kikao.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post