ASKOFU GWAJIMA APANDISHWA KIZIMBANI MARA MBILI KWA SIKU MOJA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana imemsomea mashtaka mawili yanayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (47).
Akijitetea mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha akiongozwa na Wakili Peter Kibatala, alielezea safari yake ya Arusha na namna taarifa za kutafutwa kwake na polisi zilivyomfikia na yeye kuamua kukatisha kikao na maaskofu wezake ili kurudi Dar se Salaam.
Alieleza kuwa alipofika Dar es salaam alienda moja kwa moja ofisini kwa Ofisa wa upelelezi (ZCO) Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Alieleza pia jinsi alivyoonana na ZCO na kukutana na watu 30 katika ukumbi wa ofisi hizo. Akiwa ndani ya ukumbi huo hakupata nafasi ya kukabidhi silaha kwani palikuwa na watu wengi waliokuwa wakimsonga.
Alidai kuwa “alikuwepo mtu mmoja ameshika gazeti analikung’uta, nikasikia harufu ya chaki ikinipalia nikapiga kelele, kuna kitu kinanipalia nikaanguka nikapoteza fahamu”
“Nilipozinduka nikajikuta Hospitali ya Polisi Oysterbay huku polisi mmoja akitaka kunichoma sindano bila ridhaa yangu. Baadae nilijikuta Hospitali ya TMJ na nilipohoji nimefikaje niliambiwa kuwa nimeletwa na polisi.”
Kuhusu begi lililokuwa na silaha, Gwajima alisema hakuletewa na mtu, bali alikuwa nalo alipokwenda kuripoti polisi.
Vilevile aliendelea kutoa ushahidi kuhusu risasi 17 zilizokutwa ndani ya begi, alidai kuwa risasi hizo na bunduki anazimiliki kihalali. Na kuwa aliacha silaha nyumbani bila risasi ili ikiibiwa isiwe na risasi. Kesi hiyo itasikilzwatena April 10 na 11, 2017.
Washtakiwa wengine wa kesi ya  kushindwa kuhifadhi silaha ni msaidizi wa Gwajima, Yekonia Bihagize (39), George Mzava na George Milulu. Hawa wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kumiliki bastola aina ya Berretta pamoja na risasi 20 kinyume cha sheria.
Akiwa mahakamani hapo, Gwajima alipanda tena kizimbani kwa kesi nyingine inayomkabili ambapo inadaiwa kuwa, kati ya Machi 16 na 25, 2015 akiwa Tanganyika Packers, Kawe alitumia lugha chafu kumdhihaki Askofu Mkuu wa Kanisa la Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Mahakama imetoa ahirisho la mwisho kwa upande wa mashtaka kuita mashahidi katika shtaka linalomkabili la kutoa lugha chafu.
Hakimu mfawidhi alitoa ahirisho hilo jana baada ya wakili wa Serikali Joseph Maugo kuelezea kuwa kesi ilikuja kusikilizwa lakini hawana shahidi.
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Cyprian Mkeha alisema kesi hiyo haina historia nzuri na kwamba kwa miaka miwili, upande wa mashtaka umeita shahidi mmoja tu, kwa Hivyo alitoa ahirisho la mwisho kwa upande wa mashtaka na kama hawatafunga ushahidi wao basi Mahakama itafanya itakachoweza.
Mashahidi wa upande wa ushahidi wataendelea kutoa ushahidi April 12 na 13.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post