AZANIA GROUP KUWAKALISHA TANZANIA MICHUANO YA ROAD TO ANFIELD

Timu ya Azania Group, kuwakilisha Tanzania katika mashindano ya kikanda ya Afrika Mashariki, ya Benki ya “Standard Chartered-Road to Anfield” yatakaofanyika uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park Jumamosi ya Machi 4.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Limited, Sanjay Rughani aliwaasa wachezaji wa Azania Group wajiandae kikamilifu ili waubakishe ubingwa nchini Tanzania.
Azania walipata ushindi huo kwa kuichakaza timu ya H&R Consultancy mabao ya 6-5 kwa penati katika mchezo wa fainali uliokuwa wa kukata na shoka na kufanikiwa kuipeperusha bendera ya Tanzania.
Kwa maana hiyo, Azania Group wanatarajia kumenyana uso kwa uso na washindi wa michuano hiyo kutoka nchi za Kenya na Uganda ambapo fainali hizo zitafanyika hapa nchini.
Washindi wa michuano hiyo nchini Uganda ni timu ya Cocacola na kwa upande wa Kenya mshindi ni timu ya Radio ya Capital FM.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post