BALE APIGWA FAINI NA KUFUNGIWA

STAA wa Real Madrid,Gareth Bale ataikosa michezo miwili ijayo ya La Liga kama adhabu baada ya kufungiwa kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa Jumatano iliyopita kwenye mchezo dhidi ya Las Palmas.

Bale alionyeshwa kadi mbili za njano ndani ya dakika 10 katika mchezo ambao Real Madrid ilikwenda sare ya mabao 3-3 na Las Palmas baada ya kumtembezea utemi Jonathan Viera.

Bale ambaye amesisitiza kuwa hakustahili kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo huo pia amelimwa faini ya Pauni 517 kwa kuwa ni mara yake ya pili kukumbana na adhabu hiyo katika maisha yake na mara ya kwanza tangu amejiunga na Real Madrid mwaka 2013 akitokea Tottenham.

Hii ina maana kwamba Bale hataonekana dimbani kwenye mchezo dhidi ya Eibar na ule dhidi ya Real Betis lakini atarejea kwenye mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post