BALOZI SEIF AAGANA NA MABALOZI WANAOIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MATAIFA MBALIMBALI

SHARE:

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Mabalozi Saba Wapya wa Tanzania walioteuliwa hivi karibu na Rais wa Ja...

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Mabalozi Saba Wapya wa Tanzania walioteuliwa hivi karibu na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwenda kuliwakilisha Taifa katika Nchi mbali mbali Duniani.
Balozi Seif akiwa katika Picha ya pamoja na Mabalozi wapya wanayoiwakilisha Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif waliokaa ni Balozi Pindi Chana anayekwenda Kenya, Balozi Grace Mgwano anakwenda Uganda na upande wa Kulia ya Balozi Seif ni Balozi Matilda Masuka anakwenda Korea Kusini na Balozi Fatma Rajan anakwenda Nchini Qatar. Waliosimama kutoka Kushoto ni Balozi Silima Kombo Haji anakwenda Nchini Sudan Balozi Joseph Sokoine anakwenda Nchini Belgium na Balozi Abdulla Kilima anakwenda Nchini Oman.  Picha na – OMPR – ZNZ.Picha  na - OMPR – ZNZ.

Mabalozi wanayoiwakilisha Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mataifa Rafiki Ulimwenguni wataendelea kuwa na jukumu la kuitunza Heshima ya Tanzania katika misingi imara itakayoimarisha Uhusiano mzuri uliopo kati ya pande hizo mbili.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga wakati akiwaaga Mabalozi Saba wapya wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Nchi katika Mataifa tofauti Duniani uliofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

Balozi Seif Ali Iddi alisema yapo mafungamano mazuri ya muda mrefu yaliyopo baina ya Tanzania na Nchi Rafiki ambazo Wanadiplomasia hao wa Tanzania wana kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba uwajibikaji wao unaleta tija na faida kwa mafungamano hayo katika pande zote mbili.

Balozi Seif aliwaeleza Mabalozi hao kwamba Mataifa ya Qatar, Oman, Uganda, Kenya, Belgium na Korea Kusini yamekuwa mshirika mkubwa na Tanzania katika kuimarisha Sekta za Maendeleo zinazosaidia kustawisha maisha ya Wananchi.

Alisema Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inahitaji kuendelea kuungwa mkono na Mashirika na Taasisi za Mataifa hayo ambapo Mabalozi hayo watakuwa na jukumu la kufanya ushawishi utakaopelekea azma hiyo inafanikiwa vyema.

Akigusia Nchi ya Sudan ambayo Tanzania imeamua kufungua tena Ubalozi wake baada ya kuufunga katika miaka ya 90 kutokana na hali ngumu ya uchumi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimtaka Balozi atakayesimamia Ofisi hiyo kufanya juhudi katika kuhakikisha fursa za masomo zilizokuwa zikitolewa na Nchi hiyo zinarejea kama kawaida.

Alisema Sudan ni Nchi iliyokuwa ikiifadhili na kuisaidia sana Tanzania na Zanzibar kwa jumla nafasi nyingi za masomo hasa katika fani za Elimu ya Dini ya Kiislamu na Historia.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Mabalozi wenzake Balozi wa Tanzania Nchini Oman Balozi Abdulla Kilima alisema jukumu walilokabidhiwa na kukubali kulibeba watahakikisha wanalitekeleza kwa nguvu zao zote.

Balozi Kilima kwa niaba ya wenzake wamewaahidi Watanzania kwamba watazingatia kuilinda Heshima iliyopo ya Taifa lao inayoendelea kushamiri katika Nyanja za Kimataifa.

Mabalozi aliyozungumzao nao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na kuwaaga ni pamoja na Balozi Pindi Chana anayekwenda Nchini Kenya, Balozi Silima Kombo Haji anayekwenda Sudan na Balozi Joseph Sokoine anayekwenda Nchini Belgium.

Wengine ni Balozi Abdulla Kilima anayeiwakilisha Tanzania Nchini Oman, Balozi Matilda Masuka atakayekwenda fungua Ubalozi Mpya Nchini Korea Kusini, Balozi Grace Mgwano anayekwenda Nchini Uganda na Balozi Fatma Rajab anayekwenda Nchini Qatar.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
4/3/2017.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: BALOZI SEIF AAGANA NA MABALOZI WANAOIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MATAIFA MBALIMBALI
BALOZI SEIF AAGANA NA MABALOZI WANAOIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MATAIFA MBALIMBALI
https://3.bp.blogspot.com/-jYqQ0_T-RGY/WLu7Wz0fESI/AAAAAAAAXac/56Il9I7tsGkUMYNyIXllFJVDd2ihHcy5ACLcB/s1600/BB%2B1.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-jYqQ0_T-RGY/WLu7Wz0fESI/AAAAAAAAXac/56Il9I7tsGkUMYNyIXllFJVDd2ihHcy5ACLcB/s72-c/BB%2B1.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/balozi-seif-aagana-na-mabalozi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/balozi-seif-aagana-na-mabalozi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy