BALOZI SEIF AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA TVH MJINI CHENNAI, INDIA

SHARE:

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwasha mshumaha mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Kampuni ya Ujenzi wa Nyumba za Mko...

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwasha mshumaha mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Kampuni ya Ujenzi wa Nyumba za Mkopo katika Jimbo la Chennai Nchini India. Kushoto ya Balozi Seif ni Rais wa Jumuiya ya Makampuni ya Nichan Nchini India Bwana Manohar Nichani, Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Dr. Sira Ubwa Mambora, Kayibu Mkuu Wizara ya Kilimo Nd. Juma Ali na Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini India Balozi Mohamed Hij.Kulia ya Balozi Seif ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini India Bibi Haika Msuya na Mwakilishi wa Taasisi ya Kitaifa ya mpango wa kilimo kinachotumia mbolea za Asili India Bwana Satyajit Kittur Mjini
Chennai.
Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akizungumza na Mwakilishi wa Taasisi ya Kitaifa ya mpango wa kilimo kinachotumia mbolea za Asili India Bwana Satyajit Kittur Makao Makuu ya Kampuni ya Ujenzi ya Nchini India Mjini Chennai.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Kimataifa ya Miot Dr. Malika Mohandazaz kwenye Hotelli ya Crowne Plaza Mjini Chennai kabla ya kurejea Mjini New Delhi
Mke wa Makamu wa Pili wa Raios wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akibadilishana mawazo nammoja wa Viongozi Wandamizi wa Hospitali ya Miot Mjini Chennai kabla ya Kuelekea Mjini New Delhi.

Picha na – OMPR – ZNZ.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema
Zanzibar inakusudia kubadilisha muundo wa ujenzi wa nyumba zake za
makazi na Ofisi za Serikali ili kujaribu kukabiliana na uhaba wa
maeneo ya ardhi unaovikabili Visiwa vya Zanzibar.

Balozi Seif alitoa Kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Uongozi wa
Kampuni ya Ujenzi wa Nyumba za Mikopo ya Jimbo la Chennai ya TVH
katika Jengo la Ofisi hizo liliopo Mjini Chennai Nchini India.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikizisisitiza
Taasisi zake za Umma, zile Binafsi pamoja na watu wenye uwezo
kufikiria muelekeo wa Utamaduni wa kujenga majengo ya ghorofa ambayo
mbali ya kubadilisha mandhari ya Miji mipya, lakini pia yatakidhi
mahitaji ya upatikanaji wa nyumba katika eneo dogo.
Balozi Seif alisema Zanzibar bado inahitaji kuwa na majengo ya Kisasa
yanayokwenda na wakati. Hivyo aliushauri Uongozi wa Kampuni hiyo ya
ujenzi ya TVH ya India kuangalia uwezekano wa kutumia fursa zilizopo
Zanzibar katika mpango wa uwekezaji katika Sekta ya Makaazi.

Hata hivyo Balozi Seif alisema endapo Kampuni hiyo itafikia maamuzi ya
kuanzisha Miradi yao Zanzibar ni vyema wakaangalia njia ya Ujenzi wa
Nyumba kwa kutumia Teknojia isiyohitaji Mchanga kwa vile Rasilmali
hiyo hivi sasa imepungua kwa kiasi kikubwa.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alikutana kwa mazungumzo na Mwakilishi wa Taasisi ya Kitaifa ya
mpango wa kilimo kinachotumia mbolea za Asili India Bwana Satyajit
Kittur Mjini Chennai.

Katika Mazungumzo yao Bwana Satyajit Kittur alisema India imefanikiwa
vyema katika kuimarisha Kilimo hicho na kupata heshima na tuzo mbali
mbali za Kimataifa.
Alisema zipo jitihada zinazochukuliwa na Taasisi hiyo katika muelekeo
wake wa kushirikiana na Mataifa mbali mbali zikiiwemo nchi za Bara la
Afrika zenye kutegemea uchumi wake katika Sekta ya Kilimo.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo. Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar
Nd. Juma Ali Juma alisema Wananchi wengi wa Zanzibar wamaekuwa
wakitegemea Kilimo katika kuendesha maisha yao licha ya utaalamu mdogo
wanaoutumia katika sekta hiyo.
 
Nd. Juma aliuomba Uongozi wa Taasisi hiyo ya Kitaifa ya mpango wa
kilimo kinachotumia mbolea za Asili India kufanya ziara maalum
Zanzibar ili kujionea hali halisi ya Wakulima hao na namna
watakavyoweza kusaidia Taaluma ya kuendesha kilimo kinachozingatia
tija.
 
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar B alozi Seif
Ali Iddi alisema Zanzibar iko tayari kushirikiana na Taasisi hiyo
katika muelekeo wa kuwakomboa Wakulima wake ambao wengi kati yao
bado wanaendesha kilimo kwa kutumia njia za asili.
 
Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara
ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi iko tayari kutoa kila msaada kwa
Wataalamu wa Taasisi hiyo watakaoshawishika kufika Zanzibar kuangalia
mazingira halisi ya uendeshaji wa Sekta ya Kilimo.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: BALOZI SEIF AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA TVH MJINI CHENNAI, INDIA
BALOZI SEIF AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA TVH MJINI CHENNAI, INDIA
https://1.bp.blogspot.com/-X_0XzMKVQWU/WNOem7g85WI/AAAAAAAAYgk/vxeB2wVph3oHC8a7M94DYRMUz7PBj2LEACLcB/s1600/160.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-X_0XzMKVQWU/WNOem7g85WI/AAAAAAAAYgk/vxeB2wVph3oHC8a7M94DYRMUz7PBj2LEACLcB/s72-c/160.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/balozi-seif-akutana-na-uongozi-wa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/balozi-seif-akutana-na-uongozi-wa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy