BARCELONA YAFANYA MIUJIZA NA KUWEKA HISTORIA UEFA

Barcelona imeweka historia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwa timu ya kwanza kubadili matokeo ya kufungwa magoli 4-0 katika mchezo wa kwanza na kuibuka na ushindi wa magoli 6-1 katika mchezo wa marudiano.

Timu hiyo ya Hispania ilikuwa na matokeo ya jumla ya kufungwa magoli 5-3 katika dakika ya 88 ya mchezo, lakini ikageuza matokeo kwa kufanikiwa kufunga magoli matatu katika dakika saba za mwisho wa mchezo huo uliopigwa Nou Camp.

Goli la Neymar la shuti la mpira wa adhabu na la penati lililofuatiwa na goli la Sergi Roberto katika dakika ya 95 yalitosha kuipatia ushindi usiotabirika Barcelona na kusonga mbele katika michuono hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Barcelona ilikuwa ikiongoza kwa magoli mawili kwa bila kupitia mpira wa kichwa wa Luis Suarez na Layvin Kurzawa kujifunga la pili na kisha baadaye Lionel Messi aliongeza la tayu kabla ya Edinson Cavani kuchomoa goli moja.
      Mpira wa kichwa uliopigwa na Luis Suarez ukijaa wavuni na kuandika goli la kwanza 
                   Neymar na Luis Suarez wakiondoka golini na mpira baada ya kufunga goli

               Mshambuliaji Edinson Cavani akifunga goli pekee la PSG katika mchezo huo
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post