BARCELONA YAIPA KIPIGO CHA MKONO BILA MAJIBU CELTA VIGO

Lionel Messi amefunga magoli mawili mazuri ya jitihada binafsi wakati Barcelona ikisakata kandanda la kiwango cha juu na kuichakaza kabisa Celta Vigo kwa magoli 5-0 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Hispania La Liga.

Kocha aliyetangaza nia yake ya kuachana na Barcelona, Luis Enrique, alishuhudia kikosi chake kikiinyanyasa kila idara Celta kwa kuonana vyema uwanjani na kutengeneza mashambulizi ya nguvu.

Messi alifunga goli la kwanza baada ya kutoka kasi umbali wa yadi 45, kisha baadaye akafunga goli zuri la kuubetua mpira. Barcelona iliongeza magoli kupitia kwa Ivan Rakitic na Samuel Umtiti kabla ya Messi tena kufunga.
  Luis Suarez akishuhudia mpira uliopigwa na Lionel Messi ukimshinda kipa na kujaa wavuni
          Mbrazil Neymar akiwa anauangalia mpira alioupiga ukielekea wavuni na kuandika goli
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post