BARUA YA LOWASSA KWA WALIOTIMULIWA CCM, AWAITA MASHUJAA WA KWELI

SHARE:

Kufuatia wanachama 12 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuvuliwa uanachama kutokana na kile walichosema kuwa ni usaliti, Mjumbe wa Kamati Kuu ...

Kufuatia wanachama 12 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuvuliwa uanachama kutokana na kile walichosema kuwa ni usaliti, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amewaandikia waraka huku akisema kuwa walikuwa ni mashujaa waliosimama kupigania demokrasia ya kweli.
Katika waraka huo, Lowassa pia amewakaribisha wote waliofukuzwa kujiunga na UKAWA au CHADEMA akiamini kuwa upinzani wa kweli utapatikana nje ya CCM.
Hapa chini ni ujumbe wa Lowassa kwa wote waliovuliwa uanachama CCM.
Nafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.
Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa kutoka CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwa tajwa huko katika vikao vyao.
Wamewatimua wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia demokasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama chao.Nataka kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa haki na demorasia na misingi ya utawala Bora nchini.
Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki,demokrasia na taratibu na kupinga dhulma ndani ya chama chao na nchini.Kwa kusimamia kile walichokiamini bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na uonevu.Mbegu ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini kwetu.
Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, kwamba upinzani wa kweli utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa.Nawakaribisha Chadema na UKAWA kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana,hakuna minyororo ya utumwa wa kisiasa.Kilichowapata ni sawa na kumpiga chura teke unamuongezea kasi tu.
Waje wajiunge nasi katika safari ya kuleta Demokrasia ya kweli na siasa zenye ukomavu,safari hii inahitaji umoja na mshikamano ili kufikia malengo.
Huko wanajinasibu kuwa CCM ikiyumba, nchi itayumba lakini mimi nasema kinachotokea ni kwamba, kwa jinsi CCM inavyoyumba, ndivyo wananchi wanazidi kukomaa kisiasa na kuimarika katika harakati za kutafuta mabadiliko ya kweli.
Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za msingi unaofanywa na watawala.nidhamu ya woga haina tena nafasi katika kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora.
Edward Lowassa
Mjumbe kamati Kuu chadema

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: BARUA YA LOWASSA KWA WALIOTIMULIWA CCM, AWAITA MASHUJAA WA KWELI
BARUA YA LOWASSA KWA WALIOTIMULIWA CCM, AWAITA MASHUJAA WA KWELI
https://3.bp.blogspot.com/-eWOrTzUre0A/WMZBu7H0rjI/AAAAAAAAX0E/1dP46fIc5JQ_vy13jROqmOuYZCc6S1DxACLcB/s1600/Lowassa.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-eWOrTzUre0A/WMZBu7H0rjI/AAAAAAAAX0E/1dP46fIc5JQ_vy13jROqmOuYZCc6S1DxACLcB/s72-c/Lowassa.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/barua-ya-lowassa-kwa-waliotimuliwa-ccm.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/barua-ya-lowassa-kwa-waliotimuliwa-ccm.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy