BEI YA NAFAKA TANZANIA YAANZA KUSHUKA

Bei ya nafaka hasa za mahindi na maharege katika Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa imeshuka kufuatia kuanza kwa mavuno mapya na uwepo wa nafaka hizo sokoni.
Kwa mujibu wa wafanyabiashara wa soko hilo wamesema kuwa kwa sasa bei ya gunia moja la mahindi mapya lenye ujazo wa debe sita linauzwa kati ya TZS 84,000 na TZS 90,000 ikilinganishwa na bei ya awali ambapo yalikuwa yakiuzwa kati ya TZS 100,000 na TZS 120,000.
Aidha, mahindi yaliyovunwa msimu uliopita yamekuwa adimu katika masoko mengi. Bei ya debe moja la mahindi hayo imekuwa ikiuzwa TZS 20,000 huku debe la pumba ya mahindi  kwa bei ya rejareja imefikia TZS 4,000 kutoka TZS 2,000.
mahindi
Kwa upande wa maharage, wafanyabiashara hao wameeleza kuwa bei yake imeshuka kutoka TZS 200,000 kwa gunia lenye uzito wa kilo 100 yaliyokuwa yamevunwa katika msimu uliopita. Ila kwa sasa bei ya maharage imeshuka na kufikia kuuzwa TZS 130,000 hadi 140,000 kwa gunia moja la maharage aina ya kabalima huku maharage ya njano yakiuzwa kwa bei ya TZS 150,000 na yale ya kigoma kuuzwa kwa TZS 160,000 hadi TZS 180,000 kwa gunia moja.
MAHARAGWE
Vile vile waliongeza kuwa bei ya nafaka hizo inatofautiana kutokana na ubora wake huku wakizisifia nafaka zilizovunwa katika bonde la la Ziwa Rukwa kuwa bora zaidi kuliko zilizolimwa katika bustani za Manispaa ya Sumbawanga ambayo yana punje ndogo na ni rahisi kuharibika.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post