BENZEMA AIBEBA REAL MADRID ILIYOKUWA BILA RONALDO NA BALE

Mshambuliaji nyota Mfaransa Karim Benzema amefumania nyavu mara mbili wakati Real Madrid iliyocheza bila majeruhi Cristiano Ronaldo na Gareth Bale anayetumika adhabu, ikiifunga Eibar kwa magoli 4-1.

Benzema alifunga goli lake la kwanza kwa mpira uliopanguliwa na kipa Yoel aliyekuwa ameokoa shambulizi lake la awali, na kisha kuongeza la pili akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na James Rodriguez.

Benzema alitengeneza goli la tatu kwa mpira wa krosi iliyomkuta Rodriguez aliyeunyanyua mpira juu na kumpita kipa Yoel. Goli la nne la Real lilifunga Marco Asensio baada ya shuti la Rodriguez kugonga mwamba na kumkuta mfungaji.
          Mfaransa Karim Benzema akifunga goli lake la bili katika mchezo huo jana
              James Rodriguez akifunga goli la tatu la Real Madrid katika mchezo huo jana 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post