BOMOA BOMOA BUGURUNI, KIWANDA CHA BAKHRESA CHAPEWA SIKU 5 KUBOMOA UKUTA WAKE

Wakazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam jana waliachwa na vilio wasijue pakuelekea wakati Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Shirika la Reli Tanzania (RAHCO) ilipoendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizokuwa katika eneo la hifadhi ya reli.
RAHCO iliendesha zoezi hilo ambapo ilikuwa ikibomoa nyumba zilizokuwa zimejengwa katika hifadhi ya reli ambayo ni mita 30. Zaidi ya nyumba 250 zilibomolewa ikiwa ni pamoja na ukuta wa kiwanda cha Bakhresa nao umeagizwa kubomolewa.
Ubomoaji huo wa nyumba zilizojirani na reli ya kati ni ili kupisha shughuli za ujenzi wa reli mpya ya kati ya kisasa (standard gauge) kuanza mara moja. Ubomoaji huo uliosimamiwa na RAHCO ulifanywa na kampuni ya udalali Heputwa Investment.
Akizungumza jana, Afisa Uhusiano wa  RAHCO, Catherine Moshi alisema kuwa wakazi wa eneo hilo walipewa notisi ya kwanza Aprili mwaka jana wakitakiwa kuhama eneo hilo, lakini wakakumbushwa tena Julai mwaka huo huo. Baada ya kuona kuna ambao hawajahama, walipewa tena notisi ya kuwakumbusha Februari mwaka huu kabla ya zoezi la kubomoa kuanza jana.
Mbali na wakazi hao kubomolewa nyumba zao, Moshi alisema kuwa watalazimika kuilipa RAHCO gharama walizotumia kubomoa kwa sababu watu wakivamia eneo wanatakiwa kuondoka kwa gharama zao wenyewe.
Pia RAHCO imetoa muda wa siku tano kwa Kiwanda cha Bakhresa kubomowa wenyewe sehemu ya ukuta wa kiwanda hicho uliopo katika hifadhi ya reli kutokana na eneo hilo kuwa na mitambo ya umeme.
Jiwe la msingi la ujenzi wa reli hiyo linatarajiwa kuwekwa mwishoni mwa mwezi huu ambapo litaruhusu kuanza kwa ujenzi wa awamu ya kwanza ambapo reli hiyo itaanzia Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro.
Baadhi ya waliobomolewa nyumba zao wamelalamikia kuwa hawakupewa taarifa ndani ya muda muafaka ambao wangeweza kuhama huku wengine wakieleza kuwa wamepewa taarifa kuhusu nyumba kubomolewa siku moja kabla.
WhatsApp Image 2017-03-11 at 9.34.05 PMWhatsApp Image 2017-03-11 at 9.34.04 PMWhatsApp Image 2017-03-11 at 9.34.01 PMWhatsApp Image 2017-03-11 at 9.34.00 PMWhatsApp Image 2017-03-11 at 9.33.58 PMWhatsApp Image 2017-03-11 at 9.33.12 PMWhatsApp Image 2017-03-11 at 9.33.15 PMWhatsApp Image 2017-03-11 at 9.33.17 PMWhatsApp Image 2017-03-11 at 9.33.18 PMWhatsApp Image 2017-03-11 at 9.33.20 PMWhatsApp Image 2017-03-11 at 9.33.57 PMWhatsApp Image 2017-03-11 at 9.33.10 PM

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post