BONDIA GENNADY GOLOVKIN AMDUNDA DANIEL JACOBS

Gennady Golovkin ametetea taji lake la mkanda wa middleweight baada ya kupata ushindi wa 37 mfululizo katika mapambano yake kwa kumdunda Daniel Jacobs.

Katika pambano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Madison Square Garden, Gennady Golovkin alilazimika kungojea hadi kumalizika kwa raundi zote 12 ili kupata ushindi.

Bondia mzaliwa wa Brooklyn, Daniel Jacobs ambaye amepona ugonjwa wa saratani ya mifupa, alienda chini katika raundi ya nne baada ya kupigwa ngumi nzito.

Mshindi wa pambano hilo alipatikana kwa uamuzi wa majaji ambapo Golovkin alipewa ushindi na majaji wote watatu.
                 Gennady Golovkin akimdunda ngumi iliyompeleka chini Daniel Jacobs
                     Bondia Daniel Jacobs akimpiga ngumi ya kushoto Gennady Golovkin
                      Gennady Golovkin akimpiga konde zito la mkono wa kushoto Daniel Jacobs
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post