BOURNEMOUTH YAIKOMALIA MANCHESTER UNITED NA KUTOA SARE

Manchester United imeshindwa kujikwamua kutoka katika nafasi ya sita ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Bournemouth katika dimba la Old Trafford.

Katika mchezo huo uliotawaliwa na vitendo vya ubabe baina ya Zlatan Ibrahimovic na beki Tyrone Mings, Manchester United ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa beki Marcos Rojo akinasa mpira uliopigwa na Antonio Valencia.

Hata hivyo Bournemouth walijikuta wakibakia na wachezaji 10 dimbani baada ya Andrew Surman kupewa kadi nyekundu, walipata goli lao la kusawazisha kupitia kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Joshua King baada ya Phil Jones kufanya madhambi.
                 Marcos Rojo akifunga goli lake la kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza
                        Joshua King hakufanya ajizi alitumbukiza kimiani mpira wa penati 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post