BREAKING: MBUNGE TUNDU LISSU AKAMATWA NA POLISI AKITOKA MAHAKAMANI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikiliwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu katika Kituo cha Polisi cha Kati.
Mbunge huyo amekamatwa leo asubuhi alipokuwa akitoka katika Mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu alipokuwa amekwenda kwa ajili ya kesi inayomkabili.
Lissu alikuwa amefika mahakamani hapo katika kesi ya kuchochea vurugu ambapo alituhumiwa kuwa Januari 11, mwaka huu katika kampeni za uchaguzi jimbo la Dimani aliwashawishi watu wasiridhike na wawe na nia ovu dhidi ya utawala.
Aidha, Lissu aliachiwa baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha hati ya kuondoa shtaka hilo mahakamani chini ya kifungua namba91 (1) cha makosa ya jinai akionyesha DPP hana haja ya kuendelea na kesi, mahakama ikaridhia na kumuachia.
Jeshi la Polisi halijatoa taarifa kuhusu sababu hasa ya kiongozi huyo kukamatwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post