BREAKING: NAPE NNAUYE AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUVULIWA UWAZIRI

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye amezungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni saa chache tangu Rais Dkt Magufuli alipomvua uwaziri.
Nape ambaye amezungumza na waandishi wa habari nje ya hoteli ya Protea baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumzuia kuingia ndani, amewasihi vijana kutokuwa waoga na kuendelea kutetea haki zao.
Kiongozi huyo baada ya kufika katika hoteli hiyo alizuiwa kuingia ndani kufanya mkutano na waandishi wa habari hivyo akaamua kusimama nje huku akiwa amezungukwa na waandishi wa habari.
Alianza kwa kusema kuwa anamshukuru sana Rais Magufuli kwa kumuamini kwa mwaka mmoja aliopewa kuiongoza wizara ya habari. Alisema pia hakuulizwa alipoteuliwa na hivyo hata leo alipoondolewa hawezi kuuliza.
Mimi nimeipigania CCM miezi 28, nimelala porini kuhakikisha inarudi madarakani, lakini leo watu wachache wanakuja hapa wananitolea bastola mimi, ni nani aliyewatuma ninyi? Alihoji Nape akidai kuwa kuna mtu katika mkusanyiko ule alitoa bastola.
Nnauye alikumbushi moja ya maneno aliyoyazungumza jana ambapo alisema kuwa, unapotetea haki za watu kuna gharama za kulipa na kuwa yeye yupo tayari kulipa gharama hizo kwa kutetea maslahi ya habari. Amewashukuru waandishi wa habari kwa ushirikiano mkubwa waliomuonyesha na kuwa alitamani kuendelea kufanya nao kazi.
“Nilitamani sana kuendelea kufanya kazi na ninyi waandishi wa habari lakini muda wa aliyeniweka umefika akaamua niondoke.” Alinikuniliwa Mbunge Nape akisema
Aidha, amempongeza Waziri Mteule Dkt. Harrison Mwakyembe kwa majukumu hayo aliyokabidhiwa huku akiwasihi waandishi wa habari washirikiane na kwa pamoja.
“Nape ni mdogo sana kuliko Tanzania, tusianzishe vurugu zozote bali mshirikiane na Waziri Mwakyembe.”
Nape akihitimisha mazungumzo yake alisema kuwa hana kinyongo na Rais wa Tanzania wala serikali kwa yeye allichofanya ni kutumiza wajibu wake. Lakini pia Nape amewashukuru Wananchi wa Mtama kwa wao ndio waliomuamini hata akaweza kuteuliwa kuwa Waziri.
Kuhusu vyombo vya ulinzi na usalama, Nape amevikosoa kwa namna vinavyofanyakazi huku akisema kulikuwa hakuna sababu yoyote ya msingi kuzuia mkutano wake sababu ulikuwa wa amani tu.
Wakati akiondoka kutoka hotelini hapo, Nape Nnauye alizuiwa na Kamanda wa Polisi Kinondoni lakini baada ya maongezi ya muda mfupi aliachiwa na kuweza kuondoka.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post