BREAKING: ORODHA YA VIGOGO WA CCM WALIOVULIWA UANACHAMA SABABU YA USALITI. YUMO SOPHIA SIMBA

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dodoma ambapo Mkutano Mkuu unaendelea ni kwamba, baadhi ya wananchama wa CCM wamevuliwa uanachama huku wengine wakipewa onyo kali kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni usaliti katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Miongoni wa waliofukuzwa uanachama ni pamoja na mwanachama mkongwe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba huku Adam Kimbisa akisamehewa na Emmanuel Nchimbi akipewa onyo kali. Onyo kali alilopewa Nchimbi ina maana kuwa hatoruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwa muda utakao amuliwa na chama.
Kufuatia maamuzi hayo, Sophia Simba amepoteza rasmi nafasi yake ya Ubunge wa Viti maalumu na Uenyekiti wa UWT kwani nafasi hizo zinahitaji mtu ambaye ni mwanachama wa chama aweze kuzishika. Hivyo, CCM italazimika kupeleka jina jingine Tume ya Uchaguzi kuteua mbunge wa kuziba nafasi ya Sophia, huku nafasi yake ya Uenyekiti UWT ikisubiri uchaguzi baadae mwaka huu.
Wenyeviti wa CCM Mkoa waliofukuzwa
 1. Mwenyekiti Mkoa wa Iringa,  Jesca Msambatavangu
 2. Mwenyekiti Mkoa wa Shinyanga, Erasti Izengo Kwilasa
 3. Mwenyekiti Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Rashind Madabida
 4. Mwenyekiti Mkoa Mara, Christopher Sanya
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
 1. MNEC Wilaya ya Babati Mjini, Ally Khera Sumaye- Amefukuzwa uanachama
 2. MNEC Wilaya ya Arumeru, Mathias Erasto Manga- Amefukuzwa uanachama
 3. MNEC Wilaya ya Kilwa, Ali Mchumo- Amepewa onyo kali
 4. MNEC Wilaya ya Tunduru, Ajili Kalolo- Ameachiswa uongozi
 5. MNEC Wilaya ya Singida Mjini, Hassan Mazala- Ameachiswa uongozi
 6. MNEC Wilaya ya Kibaha Vijijini, Valerian Allen Buretta- Amechishwa uongozi
Wenyeviti wa Wilaya
 1. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Omari Awadhi- Amefukuzwa uanachama
 2. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Babati Mjini, Ally S. Msuya- Amefukuzwa uanachama
 3. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya  Longido, Makolo S. Laiza- Amefukuzwa uanachama
 4. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya  Arusha Mjini, Wilfred Ole Soilel Molel- Amefukuzwa uanachama
 5. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Kondo Madenge- Amefukuzwa uanachama
 6. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya  Iringa Mjini, Abeid Kiponza- Ameachishwa uongozi
 7. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya  Ilala, Assa Simba Haroum- Ameachishwa uongozi
 8. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Hamis J. Nguli- Ameachishwa uongozi
 9. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya  Muleba, Muhaji Bushako- Amepewa onyo kali
Viongozi wa Jumuiya
 1. Mwenyekiti wa UWT Taifa, Sophia Simba- Amefukuzwa uanachama
 2. Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kigoma, Josephine Genzabuke- Amepewa onyo kali
Wajumbe wa Kamati Kuu
 1. Emmanuel Nchimbi- Amepewa onyo kali na anatakiwa kuomba radhi
 2. Adam Kimbisa- Amesamehewa
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post