CCM YATEUA MAKATIBU WA MIKOA 31, WA WILAYA 155. WAELEZA MSIMAMO WA CHAMA KUHUSU RC MAKONDA

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, akzungumza na Waandshi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam,leo. (Picha na Bashir Nkoromo)
Uteuzi wa Makatibu wa CCM Mikoa…
 1. Arusha- ­ Elias Mpanda
 2. Dar es Salaam-­ Saad Kusilawe
 3. Dodoma- ­ Jamila Yusuf
 4. Geita- ­ Adam Ngalawa
 5. Iringa- ­ Christopher Magala
 6. Kagera­- Rahel Degeleke
 7. Katavi­- Kajoro Vyahoroka
 8. Kigoma-­ Naomi Kapambala
 9. Kilimanjaro-­ Jonathan Mabihya
 10. Lindi­- Mwanamasoud Pazi
 11. Manyara- ­Paza Mwamlima
 12. Mara- ­Innocent Nanzabar
 13. Mbeya- ­Wilson Nkhambaku
 14. Morogoro-­ Kulwa Milonge
 15. Mtwara- ­Zacharia Mwansasu
 16. Mwanza-­ Raymond Mwangala
 17. Njombe-­ Hossea Mpagike
 18. Pwani-­ Anastanzia Amasi
 19. Rukwa-­ Loth Ole Nesere
 20. Ruvuma­- Amina Imbo
 21. Shinyanga- ­Haula Kachambwa
 22. Simiyu-­ Donald Etamya
 23. Singida-­ Jimson Mhagama
 24. Tabora-­ Janeth Kayanda
 25. Tanga-­ Allan Kingazi.
“Makatibu wengi (20) tuliowateua ni wapya, hatuwezi kufanya mageuzi ya kuwa na CCM mpya na upya huo usionekane. Mageuzi ni fikra” amesema Polepole.
Kuhusu suala la Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam, Polepole alisema, kwanza napenda kusema kuwa uhusiano wa CCM na vyombo vya habari ni wa kihistoria’… CCM inapenda kufuata utaratibu na ndio salama yetu kama yupo kiongozi wa chama amefanya jambo tuna utaratibu mzuri wa kuchunguza. Lakini pili, Mkuu wa Mkoa ni mteule wa Rais na anapomteua anamteua yeye peke yake na halazimiki kushauriana na mtu, hivyo badala ya kukaa na kumpangia Rais kitu cha kufanya, tumuache afanye kazi’.. “
Aidha, Humphrey Polepole akitolea ufafanuzi madai yanayoenezwa kuwa wamefanya mabadiliko kuwa Rais Magufuli ndiye atakayegombea 2020 bila kupingwa amesema kuwa, mabadiliko ya katiba waliyoyafanya katika mkutano mkuu maalum, hayakuhusu mchakato wa kumpata mgombea wa uchaguzi mwaka 2020. Hivyo tunawaomba wanachama wetu na watanzania wapuuze habari nyingine zinazoenezwa.
Katibu wa CCM itikadi na Uenezi ­Taifa
26.3.2017
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post