CHELSEA YAIVUA UBINGWA WA FA TIMU YA MANCHESTER UNITED

Chelsea imeendelea kukaza buti katika mbio za kuchukua makombe mawili Uingereza baada ya jana N'Golo Kante kufunga goli la pekee la ushindi katika kipindi cha pili katika mchezo wa FA wa robo fainali dhidi ya Manchester United katika dimba la Stamford Bridge.

Katika mchezo huo wa jana usiku kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, alilumbana na kocha wa Chelsea Antonio Conte pia alishambuliwa kwa lugha chafu na mashabiki wa Chelsea timu ambayo aliwahi kuiongoza mara mbili.

Kocha huyo mreno alikasirishwa na kitendo cha kiungo Ander Herrera kutolewa nje zikiwa zimebakia dakika kumi kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza baada ya kumchezea rafu kwa mara ya pili Eden Hazard.

Shuti la kiungo Kante katika dakika ya 51 lilifanikiwa kumaliza jitihada za kipa United David de Gea, ambaye aliokoa vyema mashambulizi ya Hazard na Gary Cahill kabla ya mapumziko. Kwa ushindi huo Chelsea itakutana na Tottenham katika mchezo wa nusu fainali.
   Refa akimuonyesha Ander Herrera kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Eden Hazard
                Kipa David de Gea akishindwa kuzuia mpira uliopigwa na N'Golo Kante
   Kocha Jose Mourinho na Antonio Conte wakizuiliwa wasidundane wakati wakitupiana maneno makali
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post