CHENGE : HAKUNA ATAKAYEKUFA NJAA BARIADI

Bariadi. Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge amewaondoa hofu wananchi jimboni mwake kuwa hakuna atakayefariki dunia kwa njaa kwa sababu vipo vyakula vya kutosha.
Chenge alitoa kauli hiyo katika Kijiji cha Mwantimba Kata ya Matongo mkoani Simiyu baada ya wakazi hao kumwomba awapatie mahindi ya msaada ili kukabiliana na njaa inayowanyemelea.
Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Kija Thelathini alimweleza mbunge huyo kuwa wananchi hulazimika kula mlo mmoja kwa sababu mazao waliyopanda yamekauka.
Mwenyekiti wa CCM wilayani humo, Juliana Mahongo alimtaka mbunge huyo kufikisha kilio chao katika mamlaka husika ili wapelekewe mahindi ya msaada watakayouziwa kwa bei nafuu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post