CHRIS BROWN AWASHANGAA TMZ KWA JAMBO HILI, ADAI KUNA WATU WANAPIGA PESA KWA AJILI YAKE

Msanii wa muziki wa Rnb nchini Marekani, Chris Brown amefunguka na kudai kuwa kuna watu wanaouza habari zake za kila siku kwenye mtandao wa TMZ.
Kupitia interview aliyofanya na kituo cha radio New York, Brown amesema anashangaa kuona baadhi ya mambo yake anayoyafanya kila siku lazima wayapate TMZ, hivyo anaamini kuna watu ambao wanapiga pesa kupitia habari zake.
TMZ ni tovuti ambayo inaelezea habari mbalimbali za watu maarufu, mtandao huo ulianzishwa Novemba 8, mwaka 2005 na kazi yao kubwa ni kununua stori na kuzisambaza.
“Kuna watu wanaofuatilia maisha yangu kuanzia naamka nadi nalala, baadhi ya mambo ambayo ninayafanya kila siku nayaona TMZ, ninaamini kuna watu wanauza habari zangu, maisha yao yanakwenda sawa kwa ajili yangu, ipo siku nitawanasa,” alisema Chris.
Tukirudi nyuma mnamo mwaka 2004, Chris Brown aliwahi kumuita CEO wa mtandao wa TMZ, Harvey Levin ‘shetani’ kwenye post ya Instagram ambayo baadaye aliifuta.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post