CHRISTIAN BELLA AANIKA HILI JUU YA MUZIKI WAKE, ADAI ANACHOTA ‘IDEA’ KWA MSANII HUYU

Mkali wa muziki wa Dance hapa Tanzania Christian Bella, ambae kwa sasa anafanya vizuri na chupa la ngoma yake “Ollah” akiwa amemshirikisha rapper kutoka Kenya Khaligraph Jones, huku chupa la ngoma hiyo likiwa limeongozwa na Hanscana.
Christian Bella amefunguka na kusema kuwa mara nyingi hata ‘idea’ ya muziki wake zinatoka kwa msanii Chris Brown kutoka Marekani na kusema ni kati ya wasanii ambao anasikiliza sana kazi zao.Christian Bella amedai kuwa anapenda kusikiliza sana kazi za Chris Brown kwanza ni kutokana na ukweli kwamba anampenda msanii huyo lakini pia kingine ni kutokana na majina yao kufanana.
“Mimi kusema kweli sina ‘Role model’ bali mimi napenda muziki mzuri lakini kwa kizazi chetu ukiangalia kwa nje nampenda sana Chris Brown na nasikiliza sana kazi zake, kwa sababu kwanza tunaendana majina ( CB )  Christian Bella, Chris Brown, yaani na mimi ni Breezy vile vile.
Aliongeza, “Yaani jamaa ana flow flani ambazo mimi mwenyewe nikimsikiliza nasikia raha lakini hata njia zake pia na feeling zake naposikiliza huwa zinanipa idea, zinanisaidia idea za kuimba lakini huwezi kuelewa kwamba kuna flow flani kwenye kazi zangu kupitia kumsikiliza Chris Brown ndiyo niliweza kuzipata” alisema Christian Bella ndani ya EATV.
Mbali na hapo Christian Bella amesema kwa wasanii wa bendi, msanii anayemkubali na kusikiliza sana kazi zake ni Koffi Olomide, kwani anadai msanii huyo amefanya mambo makubwa sana kwenye muziki wa dansi nchini DRC.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post