DIAMOND AMALIZA RASMI MGOGORO KATI YAKE NA ALIKIBA

Mwanamuziki Diamond Platnumz ametangaza rasmi leo kuwa hana mgogoro wowote na Alikiba huku akivitaka vyombo vya habari kuacha kuzusha habari za kuwa wao wawili hawaelewani.
Akizungumza leo akiwa Clouds Tv, Diamond amesema kuwa tangu zamani hakuwahi kuwa na ugomvi na Alikiba na kwamba ni mambo tu yanayozuswa mtaani ili ionekane kama wawili hao hawaelewani lakini kiukweli hawana ugomvi.
Mimi nimefahamiana na Ali tangu hata sijatoka, ule wimbo wake wa matonge (Usiniseme) mimi ndio nilimpa wale ‘dancers’ nikamwambia watafanya kiti kizuri. Wakati mimi ndio naanza muziki nilikuwa nikimpigia simu kumuomba msaada, na hata safari yangu ya kwanza kwenda Uingereza, nilikuwa nikimuuliza jinsi ya kujaza fomu ya kuomba visa, alisema Diamond Platnumz.
Alipoulizwa kama amewahi kukutana na Ali siku za karibu, Diamond Platnumz alisema kuwa, walikutana na Alikiba Nairobi ambapo walikaa na kuzungumza mambo yanayowahusu wao. Kuhusu kuweka nyimbo za Alikiba kwenye tovuti yake, Platnumz alisema hana tatizo juu ya hilo kwani hiyo ndiyo itakuwa njia salama zaidi kama nyimbo za wasanii wote zitakuwa pamoja.
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Diamond Platnumz ameandika na kuvisihi vyombo vya habari kuacha kukuza mgogoro ambao haupo kati yake na Ali.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post