DIAMOND PLATNUMZ ATAJA MISAADA ALIYOWAHI KUTOA

Mwanamuziki Diamond Platnumz amelazimika kutaja baadhi ya misaada aliyoitoa kwa jamii baada ya shabiki mmoja kuhoji msanii huyo kuvaa vito vya thamani kubwa wakati angeweza kutumia fedha hizo kusaidia watu mbalimbali wenye shida nchini.
Diamond alikuwa ameweka picha za cheni za gharama kubwa alizovaa na kusema hakuwahi kuamini kama siku moja angeweza kuvaa vitu vya gharama kubwa kiasi hicho.
Katika picha hizo mbili, moja ya cheni za mkononi zina thamani ya TZS milioni 49 wakati ile ya cheni za shingoni zilikuwa na thamani ya TZS milioni 111. Jumla ya vito hivyo vilikuwa na thamani ya TZS milioni 150.


Baada ya shabiki huyo kuhoji matumizi hayo ya fedha, Diamond alimjibu kwa kumtajia misaada aliyotoa ikiwa ni pamoja na kujengea nyumba waathirika wa mafuriko, kujenga misikiti na nyumba za watumishi wa dini.
““…..nimejenga nyumba 5 mwaka jana Iringa, misikiti miwili mmoja Morogoro pia nyingine Mtwara na madrasa Tegeta na nyumba ya Imamu mbali na sadaka mbali mbali sasa unataka nitoe hela zote sadaka nami nisifurahishe ebu niombe radhi kwa hilo.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post