DIAMOND PLATNUMZ MBIONI KUACHIA ALBAMU MPYA

MWAMKO wa kutoa albamu kwa wasanii wetu umeendelea kuongezeka kadiri siku zinavyokwenda na jana nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, ametangaza ujio wa albamu yake ya tatu inayoitwa Nothing But Bongo Fleva.

Kupitia ukurasa wake wa Instalive, mkali huyo wa singo ya Marry You, aliweka wazi kuwa albamu hiyo itatoka kabla ya ile ya kimataifa na itakuwa na nyimbo zisizopungua kumi ambazo zote zitakuwa na ladha halisi ya Bongo Fleva.
“Niko namalizia albamu yangu itaitwa Nothing But Bongo Fleva yaani hakuna chochote ila ni Bongo Fleva, itakuwa na mawe ya kibongo tu, achana na zile Make Me Sing, Kidogo, Marry You humo yatakuwa ni mawe juu ya mawe kama zile Mbagala, Nenda Kamwambie yaani ni kibongo fleva tu maumivu, visa juu ya visa ni Kiswahili, mafumbo,” alisema Diamond Platnamz.
Hatua hiyo ya Diamond kutangaza ujio wa albamu yake mpya imekuja ikiwa ni miezi michache imepita toka kundi la Navykenzo kuachia albamu yao inayoitwa Above Inna Minute (AIM).
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post