FILAMU YA ‘THE DARK TOWER’ YA IDRIS ELBA YATUPWA MBELE

Wapenzi wa filamu za mapigano na simulizi tata wamelazimika kusubiri kwa muda wa ziada kuiona filamu mpya ya Idris Elba iliyobatizwa jina la ‘The Dark Tower’, inayosubiriwa kwa hamu kuingia kwenye kumbi za sinema duniani.
Taarifa iliyotolewa na waandaaji wa filamu hiyo zimeeleza kuwa tarehe ya kuizindua rasmi na kuionesha filamu hiyo imesogezwa mbele kwa mara nyingine.
Awali, ‘The Dark Tower’ ilitarajiwa kuingia sokoni rasmi mwezi uliopita (Februari) mwaka huu, baadae ikasogezwa hadi Julai 28, na sasa imetangazwa kutupwa mbele hadi Agosti 4 mwaka huu.
‘The Dark Tower’ ni filamu iliyochukuliwa kutoka kwenye riwaya ya Stephen King ambayo ina jina hilo.

Kipande cha kwanza cha filamu hiyo kilianza kuonekana kwa mara ya kwanza Machi 27 mwaka huu, ambapo Idris Elba alionekana kama Gunslinger au Roland, na Matthew McConaughey kama villan the Man in Black.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post