FORBES: ORODHA YA MABILIONEA 25 MATAJIRI ZAIDI AFRIKA 2017

Mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa orodha ya mabilionea mwaka 2017 iliyoandaliwa na jarida la Forbes.
Utajiri wa Dangote unakadiriwa kuwa jumla ya $12.2 bilioni.
Kuna mabilionea (wa Dola) 25 mwaka huu barani Afrika, mmoja juu ya 24 waliokuwepo mwaka jana.
Wafanyabiasha kutoka Nigeria Femi Otedola na Abdulsamad Rabiu hawakufanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo mwaka huu.
Mtanzania Mohammed Dewji bado ndiye bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika, utajiri wake ukikadiriwa kuwa $1.09 bilioni.
Isabel dos Santos kutoka Angola na mfanyabiashara wa mafuta Folorunsho Alakija kutoka Nigeria ndiye mabilionea wanawake pekee katika orodha hiyo mwaka huu.
Bw Dangote Dangote, ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement inayoongoza kwa kuzalisha saruji Afrika. Anamiliki asilimia 90 ya hisa za kampuni hiyo.
Dangote Cement huzalisha tani 44 milioni za saruji kila mwaka na imepanga kuongeza uzalishaji kwa asilimia 33 kufikia 2020.
Dangote pia anamiliki hisa katika kampuni za chumvi, sukari na unga.
Mohammed Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970. Kampuni hiyo huhusika katika biashara ya nguo, unga, vinywaji na mafuta. Kampuni hiyo huendesha shughuli zake katika zaidi ya mataifa sita barani Afrika.

Mabilionea 25 wa Afrika mwaka 2017:

1. Aliko Dangote, Nigeria
Utajiri: $12.2 bilioni (TZS 27. 3 Trilioni)
2. Nicky Oppenheimer, Afrika Kusini
Utajiri: $7 bilioni (TZS 15.6 Trilioni)
3. Mike Adenuga, Nigeria
Utajiri: $6.1 bilioni (TZS 13.6 Trilioni)
4. Johann Rupert, Afrika Kusini
Utajiri: $6.3 bilioni (TZS 14.1 Trilioni)
5. Nassef Sawiris, Misri
Utajiri: $6.2 bilioni (TZS 13.9 Trilioni)
6. Christoffel Wiese, Afrika Kusini
Utajiri: $5.9 bilioni (TZS 13.2 Trilioni)
7. Nathan Kirsch, Swaziland
Utajiri: $3.9 bilioni ( TZS 8.7 Trilioni)
8. Naguib Sawiris, Misri
Utajiri: $3.8 bilioni (TZS 8.5 Trilioni)
9. Isabel dos Santos, Angola
Utajiri: $3.1 bilioni (TZS6.9 Trilioni)
10. Issad Rebrab, Algeria
Utajiri: $3 bilioni (TZS 6.7 Trilioni)
11. Mohamed Mansour, Misri
Utajiri: $2.7 bilioni (TZS 6 Trilioni)
12. Koos Bekker, Afrika Kusini
Utajiri: $2.1 bilioni (TZS 4.7 Trilioni)
13. Allan Gray, Afrika Kusini
Utajiri: $1.99 bilioni (TZS 4.4 Trilioni)
14. Othman Benjelloun, Morocco
Utajiri: $1.9 bilioni (TZS 4.2 Trilioni)
15. Mohamed Al Fayed, Misri
Utajiri: $1.82 bilioni (TZS 4.1 Trilioni)
16. Patrice Motsepe, Afrika Kusini
Utajiri: $1.81 bilioni (TZS 4 Trilioni)
17. Yasseen Mansour, Misri
Utajiri: $1.76 bilioni (TZS 3.9  Trilioni)
18. Folorunsho Alakija, Nigeria
Utajiri: $1.61 bilioni (TZS 3.6 Trilioni)
19. Aziz Akhannouch, Morocco
Utajiri: $1.58 bilioni (TZS 3.5 Trilioni)
20. Mohammed Dewji, Tanzania
Utajiri: $1.4 bilioni (TZS 3.1 Trilioni)
21. Stephen Saad, Afrika Kusini
Utajiri: $1.21 bilioni (TZS 2.7 Trilioni)
22. Youssef Mansour, Misri
Utajiri: $1.15 bilioni (TZS 2.6 Trilioni)
23. Onsi Sawiris, Misri
Utajiri: $1.14 bilioni (TZS 2.5 Trilioni)
24. Anas Sefrioui, Misri
Utajiri: $1.06 bilioni (TZS 2.4 Trilioni)
25. Jannie Mouton, Afrika Kusini
Utajiri: $1 bilioni (TZS 2 Trilioni)
-BBC
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post