GARY CAHILL KUIONGOZA ENGLAND DHIDI YA UJERUMANI

Beki wa klabu ya Chelsea Gary Cahill atawaongoza wachezaji wenzake wa England kama nahodha, katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Ujerumani ambao utachezwa usiku wa leo.
Hatua nahodha wa kikosi cha England Wayne Rooney kuachwa katika kikosi kitakachopambana na Ujerumani, kutokana na sababu za kuwa majeruhi imempa nafasi kocha mkuu wa The Three Lions Gareth Southgate kumkabidhi majukumu beki huyo.
Hata hivyo mshabiki wa soka nchini England wameshangazwa na uteuzi wa Cahill kutarajwa kuwa nahodha wa kikosi cha timu yao, huku wakitambua kuwa nahodha msaidizi aliezoeleka ni kiungo wa Liverpool Jordan Henderson na ametajwa katika kikosi cha timu yao ya taifa ambacho kitacheza dhidi ya Ujerumani.
Alipoulizwa Southgate kuhusu maamuzi ya kumpa unahodha Cahill, aliwaambia waandishi wa habari kuwa, lengo lake ni kutaka kutoa nafasi kwa kila mchezaji ili kuona ushirikino na heshima vinaendelea kutawala kikosini mwake.
Hatua ya kutajwa kama nahodha katika mchezo wa hii leo, imemfanya Cahill kuzungumza kwa kujiamini mbele ya waandishi wa habari ambapo alisema ni faraja kwake kupewa kitambaa cha unahodha cha timu ya taifa.
Alisema kwa muda mrefu amekua katika soka la ushindani na anaamini amepevuka kimwili na kiakili, hivyo hakushangazwa na maamuzi ya kocha Southgate ya kumkabidhi jukumu la kuwa kiongozi wa kikosi cha England.
England itacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Ujerumani kama maandalizi ya kuwakabili Lithuania katika mpambano wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za 2018, utakaofanyika Machi 26 jijini London.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post