GAZETI LA MAWIO LAIBWAGA SERIKALI MAHAKAMANI

Kampuni ya Victoria Media Service Ltd inayomiliki gazeti la Mawio imeshinda kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania iliyofungua kupinga uamuzi wa serikali kulifungia gazeti hilo bila kupewa nafasi ya kujitetea.
Kesi hiyo ilifunguliwa Machi 11 mwaka 2016 kufuatia gazeti hilo kufungiwa Januari 15 mwaka huo, hatua iliyochukuliwa kwa madai ya gazeti hilo kuandika habari ya kichochezi. Toleo la gazeti hilo la Janauri 5 mwaka jana, lilichapisha habari katika ukurasa wake wa mbele iliyosomeka “Machafuko yaja Zanzibar.”
Akitangaza kulifungia gazeti hilo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema kuwa gazeti hilo limekuwa likikiuka taratibu na sheria uandishi na hata walipopewa onyo, hawakusikia.
Mbali na gazeti hilo kufungiwa, Serikali ilifungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ikiwashtaki wale wote waliodaiwa kushiriki kuandika taarifa hiyo.
Walioshtakiwa kwa tuhuma za kuandika habari hiyo ni Tundu Lissu (mtoa habari), Jabir Idris (mwandishi wa habari), Simon Mkina (Mhariri Mtendaji) na Ismail Mahaboob (mchapaji wa habari).
Licha ya Victoria Media Service Ltd kushinda kesi dhidi ya uamuzi wa serikali, lakini kesi inayowakabili watuhumiwa hawa wanne bado inaendelea katika Mahakama ya Kisutu Machi 8, mwaka huu.
Kufuatia ushindi huo, gazeti hilo linatarajiwa kuanza kutoka tena mapema Alhamisi wiki hii baada ya kukosekana mtaani kwa zaidi ya mwaka mmoja.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post