HALI YAZIDI KUWA NGUMU KWA WEMA SEPETU, AGEUKWA NA WASANII WENZAKE

Muigiza Wema Sepetu amepingwa vikali na wasanii wanzake walioshiriki naye katika kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) kufuatia madai aliyoyatoa kuwa hawakulipwa fedha zao.
Wasanii hao wamesema kuwa wote walilipwa fedha zao na hata mikataba ya malipo yao ipo, na kwamba madai ya Wema kuwa wasanii wanaidai CCM si ya kweli na ni ya kupuuza.
Hayo yamesema leo na muigizaji Batuli alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Batuli naye alikuwa sehemu ya kundi la wasanii walioshiriki kampeni ya Mama Ongea na Mwanao wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Wakati Wema Sepetu akitangaza kuhama CCM na kujiunga na CHADEMA alisema kuwa wasanii walioshiriki kampeni hawajalipwa fedha zao na kuna tetesi kuwa wakienda kudai wanaambiwa wamfuate Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete.
Kabla ya wasanii hao hawajajitokeza hadharani leo, Steve Nyerere aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo alisema madai ya Wema kuwa hawakulipwa ni ya uongo kwani yeye kama kiongozi wao alihakikisha wote wamelipwa kama makubaliano yalivyokuwa.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post