HANS POPPE AELEZA SABABU YA SIMBA KUWA PAMOJA

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kikosi cha klabu hiyo kitaendelea kuwa pamoja hadi watakaporejea katika Ligi Kuu Bara.
Poppe amesema wameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha kikosi chao kinaendelea kuwa pamoja na fiti.
“Uongozi umekubaliana vijana waendelee kuwa pamoja. Tunaona ni sahihi ili kuendelea kuwa vizuri,” alisema.
Alisema Simba itaendelea na maandalizi mfululizo, ikiwezekana kucheza mechi za kirafiki zaidi na zaidi.
Kikosi cha Simba kinatarajia kurejea jijini Dar es salaam hii leo, kikitokea jijini Arusha kilipokwenda kucheza mchezo wa robo fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Madini FC, na kuibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri.
Jana jioni Simba walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mererani Stars katika Uwanja wa CCM Mererani, Arusha.
Katika mchezo huo Simba waliibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri, lililofungwa na mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast Frederick Blagnon mapema kipindi cha kwanza akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenzake, Hajja Ugando.
Wachezaji wa Simba watakua na mapumziko ya siku mbili, kabla ya kurejea katika mazoezi ya kujiandaa na michezo ya ligi kuu ambayo watacheza kanda ya ziwa wakianza na Kagera Sugar mjini Bukoba, kisha wataelekea jijini Mwanza kucheza na Mbao FC na watamaliza na Toto Africans kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post