HARAMIA HATARI WA UWINDAJI TEMBO AHUKUMIWA KWENDA JELA

Mmoja wa haramia hatari wa uwindaji tembo, anayejulikana kwa jina la “Shetani” amehukumiwa kifungo cha jela cha miaka 12, nchini Tanzania.

Haramia huyo Boniface Matthew Maliango anahusika kwa mauji ya maelfu ya tembo, kwa mujibu wa shirika la moja la uhifadhi wa wanyama pori.

Maliango alikamatwa Jijini Dar es Salaam Septemba mwaka 2015 baada ya kutafutwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Uhalifu wake wa uharamia ulipelekea kuandaliwa filamu fupi iitwayo The Ivory Game, iliyoongozwa na muigizaji Leonardo DiCaprio.

Maliango amehukumiwa pamoja na ndugu zake wa kiume Lucas Mathayo Maliango pamoja na Abdallah Ally Chaoga.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post