HARMONIZE AKIMBIA BAADA YA KUMTUSI MENEJA WA HARMORAPA

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kituo cha runinga cha East Africa (EATV) kupitia kipindi cha Friday Night Live katika ukurasa wao wa twitter imeeleza kuwa msanii Harmonize wa WCB jana aliingia mitini na kutohudhuria kipindi hicho kutokana na uwepo wa Meneja wa msanii Harmorapa na Harmorapa nje ya ofisi hiyo.
Inadaiwa kuwa baada ya kumuona meneja wa Harmorapa, msanii Harmonize aliyekuwa ndani ya gari lake alitoka na kumtusi kwa kumuonyesha ishara ya kidole cha kati ambacho husemekana kuwa ni ishara ya tusi kisha akaondoka maeneo ya studio hizo.
TAARIFA: @harmonize_tz ilikuwa awepo kwenye  muda huu, lakini ameingia mitini baada ya kumuona meneja wa @HamoRappa maeneo ya studio
Aidha msanii Harmorapa alisema kuwa alichukizwa na kukilaani kitendo hicho kwa kuwa ni cha udhalilishaji alichokifanya Harmonize kwa bosi wake.
Kufuatia kutokea kwa tukio hilo, kituo cha East Africa (EATV) kupitia ukurasa wao wa Twitter kimeomba radhi kwa watazamaji wake wote kutokana na kitendo alichokifanya Harmorapa kuonyesha hadharani tusi ambali anadai Harmonize alimtukana bosi wake.
"Tunaomba radhi kwa ishara aliyoionesha hapa @HamoRappa wakati akielezea kitendo kilichofanywa na @harmonize_tz " - @sammisago 


"Lengo letu haikuwa kuwagonganisha @HamoRappa na @harmonize_tz , bali mahojiano na @harmonize_tz kuhusu video yake mpya" - @sammisago 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post