HARMONIZE: ‘UNAJUA MIMI WCB NI KAMA CHAMBO’, AFUNGUKA JUU YA HOFU YA KUPOTEZWA KIMUZIKI

Msanii kutoka lebo ya WCB Wasafi, Harmonize amefunguka na kudai alipata hofu ya kufanyiwa fitina kwenye muziki baada ya uongozi wake kumtaka kuachia wimbo wake mpya kupitia mtandao ulioanzishwa na lebo hiyo.
Harmonize amedai kuwa uongozi wake ulipomtaka kumtanguliza kama chambo alidhani wamedhamiria kumpoteza katika ramani ya muziki ndiyo maana hawakutaka kuutambulisha wenye radio na televisheni kitu ambacho kimezoeleka.

“Unajua mimi WCB ni kama chambo kwa sababu hata lebo ilipoanzishwa mimi ndiye niliyekuwa msanii wa kwanza kusaini na nikafanya vizuri wengine wakaja, hata hivyo kwenye mauzo ya muziki kwenye mtandao nimetangulizwa mimi na namshukuru Mungu kazi zimepokelewa vizuri. Uongozi ulikuwa na mtazamo chanya tofauti na nilivyowaza.” alisema Harmonize ndani ya Planet Bongo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post