HARRY KANE AMEFUNGA MARA MBILI TOTTENHAM IKIIZAMISHA EVERTON

Harry Kane amefunga mara mbili na kuonyesha kiwango cha juu wakati Tottenham iliyopo katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza ikiifunga Everton magoli 3-2.

Mchezaji huyo Muingereza mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa anaongoza kwa ufungaji katika Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na magoli 19.

Kane alifunga goli la kwanza kwa shuti kali na kisha kuongeza goli la pili katika kipindi cha pili, kabla ya Romelu Lukaku kuchomoa moja.

Dele Alli aliongeza la tatu katika dakika ya 90, hata hivyo Enner Valencia naye akatumia dakika chache zilizosalia kabla ya mpira kuisha kuifungia Everton goli la pili.
                                           Harry Kane akifunga goli lake la pili katika mchezo huo 
                                                     Romelu Lukaku akifunga goli la kwanza la Everton 

                                                   Dele Alli akifunga kiufundi goli la tatu la Tottenham
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post