HATIMAE MANCHESTER UNITED YAKWEA HADI KATIKA NAFASI YA TANO

Manchester United imekwea hadi nafasi ya tano ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuifunga Middlesbrough kwa magoli 3-1 iliyocheza mchezo wao kwa kwanza tangu wamfukeze kocha wao Aitor Karanka.

Manchezter United ilifunga goli lake la kwanza kwa mpira wa krosi ya Ashley Young iliyomkuta Marouane Fellaini karibu na goli na kuupiga mpira kwa kichwa uliompita kipa Victor Valdes.

Jesse Lingard aliongeza goli la pili katika kipindi cha pili kwa shuti kali la mbali lililojaa wavuni, hata hivyo baadaye Middlesbrough ilisawazisha kupitia shambulizi la gonga ni kugonge ndipo Chris Smalling alipofanya makosa na kumfanya Rudy Gestede kufunga.

Hata hivyo kipa wa zamani wa Manchester United, Valdes alifanya uzembe na kuteleza wakati akijaribu kuupiga kwa mguu mpira aliorudishiwa na beki wake na kutoa fursa kwa Antonio Valencia kufunga goli la tatu.
                              Marouane Fellaini akifunga goli la kwanza kwa mpira wa kichwa
                        Jesse Lingard akifunga goli la pili la Manchester United kwa shuti kali
Kipa Victor Valdes akiteleza na kushindwa kuzuia mpira ambao Antonio Valencia aliunasa na kufunga goli la tatu
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post