IAEA WAKUTANA KUPITIA SHERIA ZA MIONZI

Na Mahmoud Ahmad Arusha
WAKUU wa sheria wa nchi wanachama wa shirikisho la nguvu za Mionzi  ulimwengini, IAEA, wameanza kongamano la siku tano la kujikumbusha na kupitia sheria mbalimbali za  matumizi ya mionzi  kwa lengo la kudhibiti madhara yanayotokana na matumizi yasiyo salama ya mionzi .
 Wakuu hao wa sheria na wataalamu, wao kutoka nchi 35 za ukanda wa Afrika zikiwemo, Aljeria, Angola, Benini, Burkinafaso,Cameroon ,DRC congo, Misri, ,Ghana, Kenya, Libya, Mali, Morocco,Namibia, Niger, Nigeria, Senegal, Afrika kusini, Sudan, Tunisia Uganda na wenyeji Tanzania wanapigwa msasa ili kusimamia na kuhakikisha sheria za matumizi ya mionzi inazingatiwa katika matumizi yake.
Akifungua kongamano hilokwenye hotel ya Naura Spiring, jijini Arusha, Mkurugenzi mkuu wa tume ya mionzi, Brigedia Jeneral , Flugence Msafiri, amesema nchi hizo zina jukumu la  kuhakikisha mionzi haisababishi madhara ya aina yeyote na kusisitiza matumizi salama ya mionzi kwa kuzingatia sheria  na usalama wa mazingira.
Amesema mionzi pia hutumika kuzalishia  Nyukilia inatumika kwenye matumizi mbalimbali ikiwemo kuzalishia nishati ya umeme, kutayarishia mitambo ya kuhifadhia mazao ya kilimo, matibabu hospitalini ,viwandani na migodini .
Msafiri,amesema Tume ya Nishati  ni taasisi ya serikali  iliyopewa jukumu la kusimamia na kudhibiti matumizi salama ya mionzi ili kulinda wananchi,mazingira na viumbe wengine ikiwemo wanyama.
Msafiri,amesema tume hiyo ilianzishwakwa sheria ya bunge namba 7 ya mwaka2003 hivyo tume kwa kushirikiana na shirika la nguvu za Atomiki Duniani inaeendesha kongamano hilo   la kikanda ,linalo husu sheria za nyukilia kwa nchi wanachama washirika la nguvu duniani ambapo  lengo ni kuwapatia washiriki uelewa wa masuala ya sheria za nyukilia  na kuangalia mfumo uliopo  wa sheria katika nchi wanachama  ili kuongeza tija  kwenye mfumo wa udhibiti wa mionzi
 .
Amesema msisitizo ni kuhakikisha kila nchi inazingatia matumizi sahihi ya Mionzi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokea wa kati wa kuitumia.
Amesema kongamano hilo linalenga kuwajengea uelewa zaidi wa sheria za mionzi ya kuzalishia nyukilia isiweze kutumika kinyume  na hivyo kusababisha madhara  kwa binadamu, mazingira nawanyama.
Msafiri, amesema inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050 matumizi ya nyukilia yatakuwa ni makubwa mno kutokana na kuwa ni chanzo cha uhakika cha kuzalisha  umeme .
Kwa upande wake Josephini Sinyo,kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa Kenya, amesema nchi yao inahimiza matumizi ya nyukilia kwaajili ya kuzalishia umeme kwa kuwa nyukilia ni chanzo cha uhakika cha nishati hiyo ya umeme.
Amesema vyanzo vingine vikiwemo, upepo na maji imegundulika kuwa sio vyanzop vya kutegemewa hasa wakati wa kiangazi maeneo mengi yanakumbwa na ukame hivyo kuathiri uzalishaji wa umeme unaotokana na maji.
 
Amesema bodi ya nyukilia nchini Kenya, inaelezea maendeleo ya sheria na mwelekeo  walionao ili kuwezesha mradi huo wa nyukilia  kuweza kutumika nchini humo.
 Aidha amesema kutokana na  wananchi kutokuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu maumnizi ya nyukilia nchini humo watatafuta utaratibu wa kutoa elimu kwa umma kutambua kuwa nyukilia wanayoihitaji ni ya kuzalisha umeme na kamwe haihusiki na maswala ya kutengenezea silaha za kivita
Kwa upande wake afisa uhusiano wa  kongamano hilo linalenga zaidi kuwakumbusha wanasheria usimamizi wa sheria za kutoa na kudhibiti  vyanzo vya mionzi na itatawaliwa na majadiliano kisha kufikia maadhimio  kuhusu matumizi ya mionzi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post