IBRAHIMOVIC AWASHUSHA PRESHA UNITED

Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic amethibitisha kuwa yupo katika mazungumzo na klabu yake ya Manchester United kuhusu kuongeza mkataba wa mwaka mmoja kufuatia kiwango kizuri alichokionyesha.
Mshambuliaji huyo kutoka Sweden alisaini mkataba wa mwaka mmoja tu kuingia Man Utd akitokea Paris Saint – German katika msimu wa joto/kiangazi uliopita.
Amekuwa akihusishwa na habari za kutaka kutimkia Napoli au LA Galaxy lakini amethibitisha kufanya mazungumzo ya kutaka kuongeza mkataba mwingine.
“Ngoja tuone ila tunafanya mazungumzo, nina nafasi ya kuongeza mwaka mmoja, nataka kufanya vizuri kwa muda nitakao kuwepo hapa. Ngoja tuone itakavyokuwa” alisema Ibrahimovic.
Aliongeza kuwa anajivunia kuwa mchezaji wa Manchester United kwakuwa watu wengi wanatamani nafasi hiyo. Alisema watu wananihitaji awe katika klabu hiyo ambayo aliitaja kama klabu bora zaidi ya Uingereza.
Mkongwe huyo amefanya vizuri katika msimu wake wa kwanza akiwa na United akipachika mabao 26 kwenye mashindano yote huku mabao mengi akipachika katika ligi kuu nchini Uingereza.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post