IDRIS SULTAN AMTAJA MREMBO ANAYEWEZA KUMTEKA MAZIMA

MSHINDI wa Big Brother Africa mwaka 2014 na mchekeshaji, Idris Sultan, ameendelea kujipatia umaarufu tangu alipoibuka kidedea wa shindano hilo lililofanyika nchini Afrika Kusini na hivyo kujikusanyia mashabiki lukuki ndani na nje ya nchi.
Kwa sasa kijana huyo ni mtangazaji wa Radio Choice FM, lakini pia akiwa ni msanii wa filamu za kibongo anayefanya vema na kazi yake mpya ijulikanayo kwa jina la ‘Karibu Kiumeni’.
BINGWA hivi karibuni lilikutana na Sultan na kupiga naye stori kuhusu maisha yake na kazi zake kwa ujumla.
BINGWA: Umezoeleka kuwa wewe ni mchekeshaji, unawezaje kuigiza filamu za ‘siriazi’?
IDRIS: Ni kipaji tu ambacho ninacho na kufanya mazoezi ya mara kwa mara, kwa sasa nina uwezo wa kufanya filamu za ‘siriazi’ na za uchekeshaji.
BINGWA: Kwenye filamu yako ya kwanza ya ‘Karibu Kiumeni’ umecheza kama nani?
IDRIS: Nimecheza kama jambazi na kijana anayefanya biashara haramu ya dawa za kulevya.
BINGWA: Umewahi kutumia dawa za kulevya kwenye ujana wako au kufanya biashara ya dawa za kulevya?
IDRIS: Sijawahi kutumia dawa za kulevya za aina yoyote na wala sijawahi kufanya biashara ya namna hiyo tangu nazaliwa.
BINGWA: Unatoa ushauri gani kwa jamii na watu wanaotumia dawa za kulevya?
IDRIS: Dawa za kulevya ni hatari kwa afya zetu na Watanzania wanajua, lakini kuna baadhi ya watu ni ving’ang’anizi bado wanaiga tabia za nje ya nchi na kutumia dawa za kulevya, Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana kama tutakubali kubadilisha mfumo wa maisha yetu na kufanya kazi kwa bidii ili kujenga Taifa letu kwa kutumia akili na vipaji tulivyojaliwa.
BINGWA: Vipi kuhusu mahusiano yako ya kimapenzi na mwanadada Wema Sepetu?
IDRIS: Mahusiano ya kimapenzi mimi na Wema Sepetu yamekwisha muda sana na kila mtu anafanya mambo yake.
BINGWA: Tangu kuachana na Wema ni muda gani umepita?
IDRIS: Ni mwaka sasa.
BINGWA: Vipi kuhusu kupigiana simu na kupeana ushauri wa mambo mbalimbali?
IDRIS: Kuhusu kupigiana simu na kupeana ushauri hapana, lakini kama tukikutana sehemu tunaongea kawaida na maisha yanasonga mbele.
BINGWA: Vipi kuhusu mpenzi wako wa sasa ni nani, mbona hatukuoni naye kama ilivyokuwa zamani wewe na Wema Sepetu?
IDRIS: Nimeamua kuishi tofauti na maisha ya zamani, sitaki kuweka wazi mahusiano yangu kwa sasa.
BINGWA: Kwa nini hutaki kuweka wazi mahusiano yako, ni kitu gani unaogopa au unaogopa kuibiwa mpenzi?
IDRIS: Aaaah! ‘kicheko’ kitu ambacho kinanifanya nisiyaweke wazi mahusiano yangu ya sasa ni kutokana na watu kufuatilia maisha yangu ya kimahusiano kuliko kazi zangu, kila mara utasikia Idris leo kafanya vile na kesho vile kuhusu mapenzi tu.
Sipendi kuongeleka zaidi kuhusu maisha yangu ya kimapenzi, napenda mashabiki zangu waniongelee kuhusu maisha ya kazi zangu.
BINGWA: Kwenye maisha ya mahusiano kuna vitu ambavyo unavizingatia kama mwanamume ili kuwa na mpenzi, je, ni vitu gani unaviangalia zaidi kutoka kwa msichana ambaye unataka kuazisha naye mahusiano?
IDRIS: Napenda kuwa na mdada kwenye mvuto zaidi, tena anayejua kupendeza, nikisema kupendeza namaanisha kuanzia mavazi hadi ‘make up’ zake.
Tena awe mdada mzuri kwa sababu napenda kuwa na watoto wazuri, hata ikitokea nimempa mimba tuzae watoto wazuri.
BINGWA: Ni kitu gani ambacho msichana asipokiweza kukifanya huwezi kuwa naye kwenye mahusiano?
IDRIS: Msichana ambaye hawezi kuongea lugha ya kigeni ‘Kiingereza’ siwezi kuwa naye kwenye mahusiano, napenda kuwa na mtu ambaye anajua kuongea lugha hata mbili, ikiwamo Kiswahili na Kiingereza au zaidi ya lugha hizo.
BINGWA: Unapendelea kufanya nini pindi ukiwa na msongo wa mawazo?
IDRIS: Mara nyingi nikiwa na msongo wa mawazo napenda kuendesha gari muda wa usiku wa manane au kufanya kazi za nyumbani, ikiwamo kupika.
BINGWA: Unaweza kuwa na mahusiano ya kimapenzi zaidi na msichana mmoja?
IDRIS: Hapana, siwezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na zaidi ya msichana mmoja, kwani ninayaheshimu mapenzi kuliko kitu chochote.
BINGWA: Ni sahihi kushikiana simu na mpenzi wako?
IDRIS: Sina jibu sahihi, lakini sipendi kushika simu ya mpenzi wangu kwa sababu kila mtu ana uhuru na simu yake.
BINGWA: Ni kitu gani unakikosa kutokana na ustaa wako?
IDRIS: Watu wanashindwa kuniamini kwa mfano, nikimtaka mdada nikimwambia nampenda yeye anahisi ninamtania au ninachekesha, kutokana na kazi yangu ya uchekeshaji kuna kipindi ninajikuta nakosa hadi mtu wa kuwa naye kwenye mahusiano.
BINGWA: Asante sana, Idris mashabiki zako wategemee nini kutoka kwako?
IDRIS: Asante pia. Mashabiki zangu na wapenzi wa kazi zangu  wakae mkao wa kula, kwani kuna kazi nyingi kutoka kwangu zinakuja.

bingwa
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post