ISOME BARUA INAYODAIWA NI YA TUNDU LISSU ALIYOANDIKA AKIWA KITUO CHA POLISI

Mbunge wa Singida Mjini, Tundu Lissu amekamatwa leo asubuhi akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo haijafahamika sababu za kukamatwa kwake.
Hapa chini ni barua inayodaiwa kutoka kwa kiongozi akiwa katika kituo cha Polisi.
Mawakili wenzangu salaam. Naandika haya nikiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar. Kama ilivyokuwa kwa Dkt. Martin Luther King Jr., all those years ago, hii ni Barua yangu Kutoka Mahabusu ya Polisi Dar.
Nimekamatwa nikiwa ndani ya  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Nilikwenda kama wakili katika kesi ya Jamhuri dhidi ya Bi. Shakira Abdallah Makame mbele ya Mh. Mwijage, PRM. Mimi ni wakili wa Bi Shakira anayeshtakiwa kwa cybercrimes na kesi yake ilikuwa inakuja leo kwa kusikilizwa.
Nilikwenda pia kwa ajili ya kesi yangu iliyotokana na kukamatwa kwangu bungeni Dodoma mwezi uliopita. Kesi hiyo imefutwa rasmi leo baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali kuiambia Mahakama kwamba serikali haina nia tena ya kuendelea na mashtaka hayo. Sikutoka hata nje ya ukumbi wa mahakama nikakamatwa tena.
Sijaambiwa kosa nililofanya hadi sasa, licha ya kudai hilo. Binafsi nahusisha kukamatwa kwangu na siasa za Uchaguzi wa TLS wiki ijayo. Jana nilituma mawasiliano kuhusu njama za kunizuia kugombea kwa kunifungulia kesi kwa madai kuwa sina ‘good standing.’ Sasa wameamua kutumia polisi.
Kwa vyovyote vile itakavyokuwa, hili ni shambulio kwa electoral integrity ya TLS. Serikali hii ya Rais John Pombe Magufuli inataka kuingilia na kuvuruga Uchaguzi wa TLS. Ilishatangaza msimamo wake hadharani, sasa ni utekelezaji wa msimamo huo.
Kama kuna chembe ya professional pride, integrity and independence iliyobaki ndani ya TLS huu ndio wakati wa kuionyesha. TLS isikae kimya kwenye jambo hili. We’ll be completely and forever discredited if we bury our collective heads in the proverbial sand and pretend this arrest does not concern us.
It does concern us. Massively. And so my call to the TLS leadership and my fellow lawyers is this: stand up and be counted. Take a position publicly whichever way you want, but for our own sakes please don’t keep quiet. Our Regional Chapters should also do the same. As should the EALS.
You don’t have to love me. You don’t have to support my candidacy. But for god’s sake take a position. This is an attack on the very soul of an independent professional Bar Association: the integrity of our independent electoral system. We’d put up the stiffest resistance against this assault on our independence or we’d forever shut up!!!!
I wish you all the very best for next week and for the future struggles ahead.
Tundu Lissu
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post