JINA LA MAMA SALMA KIKWETE NA HALIMA MDEE YALIVYOTUMIKA KUTAPELI FEDHA

Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro ametoa tahadhari kwa wananchi kuhusu uwepo wa Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos), kinachotapeli watu fedha kwa kutumia majina ya watu maarufu nchini hasa viongozi wa kisiasa.
Kamishna Sirro aliyasema hayo jana kwa waandishi wa habari ambapo alieleza chama hicho kinachofahamika kwa jina la Focus Vicoba na kutumia tovuti za http://www.vicobaloanstz. wapka-mob” www.vicobaloanstz. wapka-mob, hutumia majina ya viongozi serikalini na watu maarufu kwa nia ya kuwatapeli wananchi.
Watu hao ambapo wanadaiwa wanatengeneza akaunti zenye majina ya uongo kwenye mitandao ya kijamii, huwasawishi watu waone kuwa wanaweza kupata mikopo kwa gharama nafuu na kwa haraka zaidi kupitia mtandao. Katika akaunti hizo na kwenye tovuti za mitandao hiyo imebainika kuwa wameweka namba za uongo ambazo si za watu wanaodai ni zao.
Baadhi ya namba zilizonaswa ni 0757 308381 na 0768 199359 ambazo si za Mama Salma Kikwete wala Reginald Mengi kama ambavyo matapeli hao walivyodai.
Miongoni mwa majina ambayo Kamishna Sirro alisema yanatumika zaidi kutapeli ni pamoja na jina la mke wa Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Salma Kikwete, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
Kamishna Sirro alisema kuwa mwaka jana Disemba 16 walifanikiwa kumkamata Boniface Ojwando (27) anayetuhumiwa kujioatia fedha kwa njia ya udanganyifu na tayari amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Sirro ametoa rai kwa wananchi kutokuwa wepesi kumuamini mtu wasiyemfahamu hasa kwenye mitandao linapokuja suala linalohusu masuala ya fedha kwani watu wengi wamelalamika kutapeliwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post