JOSE MOURINHO ACHEKELEA MATOKEO YA SARE

Meneja wa kikosi cha Man Utd Jose Mourinho amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na wachezaji wake ya kupambana na kufanikiwa kupata bao la ugenini katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora wa Europa League, dhidi ya FC Rostov ya Urusi.
Kiungo mshambuliaji kutoka Armenia Henrikh Mkhitaryan alifunga bao la Man Utd katika dakika 35, kabla Aleksandr Bukharov hajaisawazishia Rostov dakika ya 53.
Jose Mourinho aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kikosi chake kilicheza vizuri na imekua faraja kwa kila mmoja wao kuondoka katika uwanja wa ugenini wakiwa na matokeo ya sare.
Mourinho alisema inapendeza kuwa na bao la ugenini, ambalo ana imani litawasaidia katika mchezo wa mkondo wa pili ambao utachezwa juma lijalo kwenye uwanja wa Old Trafford.
Katika mchezo huo, Man Utd watatakiwa kusaka ushindi na ikishindikana watalazimika kutafuta angalau matokeo ya bila kufungana ili kufanikisha safari ya kutinga kwenye hatua ya robo fainali.
Hata hivyo FC Rostov kama watapata sare ya zaidi ya bao moja ama ushidni wowote katika mchezo huo, watakua wamefaulu kutinga katika ya robo fainali.
Matokeo ya michezo mingine ya hatua ya 16 bora ya Europa League.
APOEL Nicosia 0 – 1 Anderlecht
FC Koebenhavn 2 – 1 Ajax
Celta Vigo 2 – 1 FC Krasnodar
Gent 2 – 5 Genk
Lyon 4 – 2 Roma
Olympiacos 1 – 1 Besiktas
Schalke 04 1 – 1 Borussia Moenchengladbach
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post